Pompeo ashitakiwa juu ya mauzo ya haraka ya silaha kwa Imarati
Kesi imewasilishwa katika Mahakama ya Federali ya Marekani kuzuia hatua ya Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo, Mike Pompeo, ya kuuzia silha aUmoja wa Falme za Kiarabu bila kufuata taratibu zinazotakiwa, katika wiki za mwisho za urais wa Donald Trump.
Faili hilo la kupinga mauzo hayo ya haraka ya silaha kwa Imarati limewasilishwa mahakamani na Kituo cha Masuala ya Sera za Kigeni cha New York, ambacho kinapinga mauzo hayo yenye thamani ya dola bilioni 23.
Kituo hicho kimesema Pompeo hakufuata kanuni za mauzo ya silaha, na badala yake aliharakisha mchakato wa mauzo hayo ya silaha kwa Imarati kinyume cha sheria.
Kituo hicho cha utafiti chenye makao yake mjini New York kinaitaka Mahakama ya Federali ya Marekani itoe amri ya kusimamishwa haraka iwezekanavyo mauzo hayo.

Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zinanunua silaha mbalimbali kutoka Marekani na katika nchi nyingine za Magharibi kwa ajili ya kuwaulia wananchi wasio na ulinzi wa Yemen.
Nchi nyingi za Kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia, Imarati, Bahrain, Kuwait na Misri kwa mwaka hununua silaha za mabilioni ya dola kutoka Marekani.