EU yaitaka serikali ya Biden isipoteze muda, iokoe JCPOA
(last modified Thu, 21 Jan 2021 04:31:34 GMT )
Jan 21, 2021 04:31 UTC
  • EU yaitaka serikali ya Biden isipoteze muda, iokoe JCPOA

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ameutaka utawala ujao nchini Marekani wa Joe Biden uokoe muda kwa kujiunga upya na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, badala ya kutaka kufanyike mazungumzo mapya juu ya mapatano hayo ya kimataifa.

Josep Borrel ametoa mwito wa kufunguliwa ukurasa mpya katika uongozi wa Marekani baada ya kufikia tamati utawala wa Donald Trump na kusisitiza kuwa: Kuna mambo mawili muhimu, kwanza ni Marekani kurejea katika Makubaliano ya Tabianchi na pili kujiunga upya na mapatano ya JCPOA, na hayo yakifanyika, dunia itakuwa pahala salama na bora zaidi.

Alipoulizwa na wanahabari kuhusu hatua za mwanzo zinazopaswa kuchukuliwa na serikali ya Biden, Mkuu wa Sera za Nje wa EU amebainisha kuwa, hatua muhimu ya kwanza kwa Marekani ni kuacha kuwatishia kwa vikwazo wale wote wenye uhusiano mzuri wa kiuchumi na Iran.

Viongozi wa nchi za Ulaya wamekuwa wakisisitiza kuwa, vikwazo shadidi vya Trump dhidi ya Iran vimeifanya Tehran ipunguze uwajibikaji wake katika makubaliano ya JCPOA. 

Hatua ya Trump ya kuiondoa US katika JCPOA ilikosolewa na hata waifitaki wa Washington

Mnamo tarehe 8 Mei 2018, Trump alitangaza uamuzi wa upande mmoja wa kuitoa nchi yake katika makubaliano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA sambamba na kurejesha vikwazo vya nyuklia vya nchi hiyo dhidi ya Iran.

Hatua hiyo iliyo kinyume cha sheria ya Trump ilikosolewa vikali katika uga wa kimataifa na hata ndani ya Marekani yenyewe.

 

Tags