Mjumbe wa Venezuela ashindwa kuvumilia jinai za Israel
(last modified Sun, 08 May 2016 03:47:35 GMT )
May 08, 2016 03:47 UTC
  •  Mjumbe wa Venezuela ashindwa kuvumilia jinai za Israel

Wawakilishi wa Venezuela na utawala wa Kizayuni wa Israel wameshambuliana kwa maneno katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na Palestina.

Shirika la habari la Anadolu la nchini Uturuki limeripoti kuwa, malumbano hayo yalitokea siku ya Ijumaa wakati kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilipokuwa kinajadili kadhia ya Palestina ambapo Rafael Ramirez, mwakilishi wa kudumu wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa alishindwa kuvumilia uongo jinai na uongo unaoenezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuamua kuushambulia vikali kwa maneno.

Ramirez aliulaumu vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendelea kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina na kuzidi kukanyaga sheria za kimataifa na kuhoji kwa kusema, hadi lini Israel itaendelea kufanya jinai dhidi ya Wapalestina?

Mara baada ya kutolewa matamshi hayo na Ramirez, mwakilishi wa utawala wa Kizayuni alianza kupayuka na kumtuhumu Ramirez kuwa anawachukia Mayahudi.

Licha ya utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya jinai za kila namna dhidi ya Wapalestina, lakini hauko tayari kusikia watu wakiulamumu hata kwa maneno tu utawala huo dhalimu kwa jinai zake za kutisha.

Tags