Takwa la Amnesty International la kuwekewa vikwazo vya silaha Israel
(last modified Wed, 23 Oct 2024 02:22:23 GMT )
Oct 23, 2024 02:22 UTC
  • Takwa la Amnesty International la kuwekewa vikwazo vya silaha Israel

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limezitaka nchi za Ulaya kuuwekea vikwazo vya silaha utawala haramu wa Israel.

Shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binadamu limetangaza kuwa: Tunashuhudia kwamba, licha ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon na Gaza, lakini nchi za Ulaya zinaendelea kutuma silaha kwa utawala huo. Tunataka Israel isusiwe kikamilifuu kiuchumi kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na utawala huo.

Katika sehemu nyingine ya taarifa yake hiyo Amnesty International imesema: Mataifa ya dunia yanapaswa kuiwekea vikwazo vya silaha Israel. Vikwazo hivi havipaswi kujumuisha tu vikwazo vya silaha, bali baadhi ya bidhaa zinazotumika katika uzalishaji wa silaha hizi pia zinapaswa kuwekewa vikwazo. Miongoni mwa mataifa ya Ulaya, Ujerumani kwa kudhamini 30% ya silaha za utawala vamizi wa Israel imekuwa na mchango mkubwa wa kuendelea mauaji ya Wapalestina huko Gaza na mauaji ya raia wa Lebanon.

Baada ya kuanza vita vya Gaza kufuatia oparesheni ya Kimbunga ya Al-Aqswa tarehe 7 Oktoba 2023 na jinai zisizo na kifani za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu madhulumu wa Gaza hususan mauaji ya kimbari na utumiaji njaa kama silaha na kuzusha baa la njaa, suala la kuiwekea vikwazo vya silaha Israel limechukua wigo mpana sambamba na kuongezeka mashinikizo na kutengwa utawala wa Kizayuni wa Israel.  Miito na harakati za kuwekewa vikwazo Israel zimefikia katika ngazi ya kimataifa ambapo taasisi na nchi nyingi zimekuwa zikitoa mwito wa kuwekewa vikwazo vya silaha Israel.

Maandamano ya kutaka kutengwa na kususiwa Israel

 

Hata hivyo takwa hili limekuwa likipuuzwa na Marekani ambayo ni muungaji mkono mkuu wa Israel pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya, hasa Ujerumani. Pamoja na hayo, wananchi wa nchi nyingi za Ulaya wamechukua misimamo mikali dhidi ya utawala wa Kizayuni na kwa kuandaa maandamano na mikusanyiko ya watu pamoja na migomo ya kuketi, wametaka kusitishwa uvamizi na misaada ya Israel kwa watu wa Gaza.

Umoja wa Mataifa pia unataka kuzidisha vikwazo dhidi ya Israel ili kuishinikiza ikomeshe vita huko Gaza.

Michael Fakhri, ripota maalum wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki ya chakula, alisema katikati ya Juni mwaka huu kwamba: Tunachohitaji sasa ni Israel kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na kisiasa.

Sisitizo la ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki ya chakula juu ya ulazima wa vikwazo vya kiuchumi na kisiasa dhidi ya Israel linatolewa kutokana na kutokuwa na natija mashinikizo ya kisiasa na kupuuzwa na Tel Aviv matakwa ya kusimamisha vita vya Gaza na mauaji ya halaiki yanayofanyika kwa lengo la kuwaangamiza watu wanaodhulumiwa wa Ukanda huo.

Utawala wa Kizayuni wa Israel sio tu kwamba unashuhudia ongezeko ambalo halijawahi kushuhudiwa la vikwazo dhidi ya taasisi zake tanzu vikiwemo vyuo vikuu na vituo vyake vya kisayansi, bali hivi sasa vikwazo hivyo vimechukua wigo mpana na kufikia kiwango cha ushirikiano wa kijeshi na silaha kati ya makampuni ya Magharibi na Israel.

Zaidi ya Wapalestina 43,000 wameuawa shahidi tangu Israel ianzishe mashambulio ya kinyama katika Ukanda wa Gaza Oktoba 2023

 

Katika mlolongo huo, hata nchi za Ulaya zimetafakari upya ushirikiano na makampuni ya silaha ya Israel. Shirika la Habari la Reuters likinuukuu vyanzo viwili limeripoti kuwa, Ufaransa imepiga marufuku makampuni ya Israel kushiriki katika maonyesho ya silaha za majini ya nchi hiyo.

Ripoti hii, iliyochapishwa Jumatano, Oktoba 16, inataja marufuku ya kuwepo kwa makampuni ya Israel kwamba ni ishara nyingine ya kuongezeka kwa mzozo kati ya Ufaransa na utawala ghasibu wa Israel.

Ufaransa hapo awali ilizuia makampuni ya Israel kushiriki katika maonyesho mengine ya silaha ambayo yalifanyika mwanzoni mwa mwaka huu.

Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa inasema kuwa, maadamu Rais Emmanuel Macron anataka kusimamishwa operesheni za kijeshi za Israel huko Gaza, uwepo wa makampuni ya Israel katika maonyesho ya silaha haufai.  Maonyesho haya yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 4 hadi 7 Novemba mwaka huu.

Pamoja na hayo, baadhi ya waitifaki wa Israel wa Ulaya hususan Ujerumani na Uingereza wameshikilia misimamo ya kuuunga mkono utawala wa Kizayuni na kuendelea kutuma zana za kijeshi kwa utawala huo ghasibu na hata kutetea jinai za Israel wakati wa vita vya Gaza hususan mauaji ya raia.

Kuhusiana na hilo, hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock katika mkutano wa Bunge la Shirikisho la Ujerumani Oktoba 10, wakati wa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa shambulio la Israel kwenye Ukanda wa Gaza, lilifanyika Oktoba 7, 2023, ilikumbana na radiamali kubwa.

Maandamano ya kupinga hatua ya Ujerumani ya kuendelea kuipatia silaha Israel inayofanya mauaji huko Palestina

 

Katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani alidai kuwa Hamas inajificha katika mikusanyiko ya raia na shule na kusema: Bila shaka, kujilinda kunamaanisha kuwatokomeza magaidi na sio kuwashambulia tu. Aliongeza kuwa, ni kutokana na sababu hiyo ndio maana, niliuueleza Umoja wa Mataifa kwamba maeneo ya kiraia yanaweza pia kupoteza hadhi yao ya ulinzi kutokana na magaidi kuyatumia vibaya.

Hata hivyo, msimamo huu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ulikabiliwa na majibu ya Umoja wa Mataifa. Tarehe 15 Oktoba, Francesca Albanese, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Palestina, alilaani kauli za Baerbok za kutetea mashambulizi ya Israel kwenye maeneo ya wakimbizi wa Kipalestina huko Gaza na kuonya juu ya matokeo ya kisheria ya kusaidia utawala ambao unafanya uhalifu na jinai za kimataifa.

Jambo lisilo na shaka ni kkuwa, filihali Israel inaandamwa na mashinikkizo ya kila upande ya kuitenga na kuiwekea mashinikizo na vikwazo kutokana na kutenda jina za kutisha dhidi ya wananchi wa Palestina hususan wa ukanda wa Gaza.

Tags