70% ya Wazayuni hawataki kurudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel)
Licha ya juhudi za Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni za kuwarejesha walowezi wa Kizayuni kwenye vitongoji walivyojengewa lakini matokeo ya uchunguzi yameonyesha kuwa asilimia 70 kati yao hawataki kurejea tena katika makazi hayo.
Mtandao wa Sahab umelinukuu shirika la habari la IRNA na kuripoti kuwa, kwa wiki ya tano mfululizo sasa, asilimia 70 ya Wazayuni hawafikirii kurejea katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) kutokana na kuendelea operesheni za kulipiza kisasi za Harakati ya Hizbullah ya Lebanon dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Vyombo vya habari vya Kizayuni waliwahi kukiri kuwa walowezi Kizayuni hawana hamu ya kurudi tena katika vitongoji walivyojengewa wakihofia mashambuli ya Hizbullah.
Licha ya kutangazwa habari hii, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni jana Jumanne alidai kuwa anafanya kila awezalo ili kuwarejesha Wazayuni katika vitongoji vyao.
Asubuhi ya Jumatatu tarehe 23 Septemba 2023, jeshi la Kizayuni lilifanya mashambulizi makubwa katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Lebanon, na yangali yanaendelea.
Wizara ya Afya ya Lebanon imetangaza kuwa, Walebanon zaidi ya elfu mbili wameuawa shahidi na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni nchini humo.