Msambao wa COVID-19 washadidisha baa la njaa ulimwenguni
(last modified Thu, 29 Apr 2021 08:05:39 GMT )
Apr 29, 2021 08:05 UTC
  • Msambao wa COVID-19 washadidisha baa la njaa ulimwenguni

Msambao wa virusi vya corona unaelezwa kuwa umeshadidisha baa la njaa katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Baadhi ya ripoti zinaeleza kwamba, mamilioni ya watu ulimwenguni wameongezeka katika orodha ya idadi ya watu wanaotaabika kwa baa la njaa katika maeneo tofauti ya dunia. na kwamba, yamkini hali ikazidi kuwa mbaya zaidi katika miezi ijayo.

Benki ya Dunia inakadiria kwamba, zaidi ya watu milioni 60 yumkini hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu (2021) wakakumbwa na umasikini wa kupindukia. 

Utafiti wa baadhi ya asasi unaonyesha kuwa, virusi vya corona vimeathiri pakubwa hali ya maisha ya watu katika maeneo mbalimbali ya dunia hususan sekta ya uchumi na kuyafanya maisha kuwa magumu. Aidha watu wengi wamepoteza ajira kutokana na mashirika yao kukumbwa na wimbi la ukata uliosababishwa mtikisiko wa uchumi ikiwa ni moja ya athari za COVID-19.

 

Huku hayo yakirjiri Umoja wa Mataifa  umetoa indhari kuhusiana na kutokea ukame katika mataifa ya katikati na magharibi mwa Afrika.

Mpango wa Chakula Duniani umetangaza kuwa, bei ya bidhaa za chakula katika baadhi ya mataifa zimepanda kwa asilimia 200 na kwamba, hali itazidi kuwa mbaya katika miezi ijayo.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa, watu milioni 31 hawataweza kujipatia chakula cha kutosha katika miezi michache ijayo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ukame na taathira za virusi vya corona kwa uchumi wa dunia.