Ujerumani: Mazungumzo ya JCPOA yapo katika hatua za mwisho
(last modified Tue, 08 Jun 2021 02:31:19 GMT )
Jun 08, 2021 02:31 UTC
  • Ujerumani: Mazungumzo ya JCPOA yapo katika hatua za mwisho

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema mazungumzo kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanayoendelea huko Vienna, Austria yapo katika kipindi cha lala salama.

Heiko Mass aliyasema hayo jana Jumatatu mjini Berlin na kuongeza kuwa, anaamini kuwa mafanikio yaliyopatikana kufikia sasa kwenye mazungumzo hayo yametokana na uvumilivu na imani ya Ulaya.

Amebainisha kuwa, anatumai Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaonesha irada ya kisiasa hadi pale mazungumzo hayo ya Vienna yatakapofikia tamati na kuzaa matunda.

Hii ni katika hali ambayo, Kikao cha Juni cha Bodi ya Gavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kiling'oa nanga jana Jumatatu.

Mazungumzo ya Vienna

Kikao hicho cha faragha kinahudhuriwa na wanachama 35 wa bodi hiyo ya IAEA kupitia njia ya intaneti kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona. 

Duru za habari zimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Marekani hazina azma ya kushinikiza kupasishwa azimio dhidi ya Iran katika kikao hicho cha Bodi ya Gavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Tags