Jumuiya ya Redio na Televisheni za Kiislamu yakosoa undumakuwili wa Marekani
Jumuiya ya Redio na Televisheni za Kiislamu imelaani hatua ya Wizara ya Sheria ya Marekani ya kufunga tovuti za baadhi ya taasisii za habari wanachama wa jumuiya hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Redio na Televisheni za Kiislamu imesema Wizara ya Sheria ya Marekani imefungia mitandao hiyo kwa kutegemea visingizio vya uongo.
Taarifa hiyo imesema kuwa, kuwepo katika safu ya mbele ya kukabiliana na siasa za dola la kigaidi la Marekani ni jambo la kujifaharisha na kuongeza kuwa: Suala hili ni kielelezo cha athari na nafasi muhimu ya taasisi za mawasiliiano na upashaji habari wanachama wa Jumuiya ya Redio na Televisheni za Kiislamu katika kuyatetea mataifa yanayodhulumiwa na kadhia ya Palestina.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa: Wanasiasa wa Marekani wanashindwa kustahamili vyombo vya habari vinavyofichua nyuso zao chafu kwa walimwengu na kukata mikono yao katika nchi za Magharibi mwa Asia.
Taarifa ya Jumuiya ya Redio na Televisheni za Kiislamu imesema kuwa: Marekani inatumia kisingizio cha uhuru na haki za binadamu kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine duniani na inazishinikiza na kuziwekea vikwazo nchi na taasisi mbalimbali ikifanya njama za kuziba midomo ya watu na kuwakandamiza wapigania uhuru, na vilevile inatumia sheria zake yenyewe na ukiukaji wa demokrasia kuhalalisha jinai na uhalifu wake.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Marekani na vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na dola hjilo la kibeberu vimefeli katika njama zao za kutaka kuyapotosha mataifa mbalimbali.
Jana serikali mpya ya Marekani iliendeleza sera za kiijuba ya kibeberu za nchi hiyo kwa kuzifunga tovuti za televisheni za kimataifa za IRIB ambazo ni Press TV, Al Alam na Al Khauthar. Kufuatia hatua hiyo Press TV imetangaza kuwa tovuti iliyofungwa ya presstv.com sasa inapatikana kupitia presstv.ir