Umoja wa Mataifa kuchunguza jinai za kivita huko Tigray
https://parstoday.ir/sw/news/world-i76494-umoja_wa_mataifa_kuchunguza_jinai_za_kivita_huko_tigray
Umoja wa Mataifa umeamua kufanya uchunguzi na kutoa ripoti kuhusu jinai za kutisha zinazoripotiwa kufanyika katika eneo la Tigray huko kaskazini mw Ethiopia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 03, 2021 08:34 UTC
  • Umoja wa Mataifa kuchunguza jinai za kivita huko Tigray

Umoja wa Mataifa umeamua kufanya uchunguzi na kutoa ripoti kuhusu jinai za kutisha zinazoripotiwa kufanyika katika eneo la Tigray huko kaskazini mw Ethiopia.

Ni baada ya umoja huo kutoa ripoti na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika katika eneo hilo katika kipindii chote cha vita na mapigano yanayoendelea baina ya waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) na vikosi vya majeshi ya serikali kuu ya Ethiopia.

Miongoni mwa uhalifu unaoripotiwa kufanyika katika eneo hilo ni tuhuma kwamba wanajeshi wa Ethiopia wamewabaka wanawake kwa makundi, kufanya mauaji ya halaiki na kuzuia misaada ya kibinadamu kwa raia walioathiriwa na vita. 

Serikali kuu ya Ethipoa imekanusha kuzuia misaada ya kibinadamu na kudai kuwa imewachukulia hatua wanajeshi waliokwenda kinyume cha sheria.

Tigray

Siku chache zilizopita pia serikali ya Ethiopia ilitangaza kuwa, waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) wameua makumi ya raia kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa ya serikali ya Ethiopia imeeleza kuwa, waasi hao wameua zaidi ya raia 100 katika eneo la Kombolcha na na kwamba makumi ya wengine kujeruhiwa.

Chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kimedai kuteka miji kadhaa katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na miji muhimu ya Dessie na Kombolcha katika eneo la Amhara, na kusema wapiganaji wake wanaelekea karibu na mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.