Undumakuwili wa India katika suala la kutoa uraia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i78416-undumakuwili_wa_india_katika_suala_la_kutoa_uraia
Serikali ya India imesema imewapatia uraia watu elfu tatu, ambao ni raia wa jamii za wachache katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Bangladesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 25, 2021 01:03 UTC
  • Undumakuwili wa India katika suala la kutoa uraia

Serikali ya India imesema imewapatia uraia watu elfu tatu, ambao ni raia wa jamii za wachache katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Bangladesh.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Nityanand Rai ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba, maombi ya uraia yaliyopokea wizara yake kutoka kwa watu wa jamii za wachache za Wahindu, Makalasinga na Wakristo katika nchi za Pakistan, Bangladesh na Afghanistan katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imefika 8,244.

Tangu serikali ya chama cha Kihindu cha Bharatiya Janata (BJP) mwaka 2014, kumefanyika mabadiliko ya akthari ya sheria kwa ajili ya kuwaridhisha Wahindu wenye misimamo ya kufurutu ada, mabadiliko ambayo yanakinzana na katiba ya India. Aidha katika kipindi cha utawala wa chama hiki kuna kesi nyingi ambazo hukumu zake zimetolewa kwa matashi ya kisiasa na kukanyaka haki za jamii za walio wachache hususan Waislamu.

 

Waziri Mkuu wa India Narendra Mosi ambaye serikali yake inaendesha ubaguzi dhidi ya Waislamu

Miongoni mwa sheria hizo ni ile ya mwezi Disemba 2019, ambapo serikali ya India ilipitisha sheria ya uhamiaji ambayo inaharakisha utoaji wa uraia kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ikiwa tu ni Wahindu au wa imani zingine, isipokuwa Waislamu. Hii ni katika hali ambayo, kupata uraia kwa mujibu wa katiba ya India ni haki inayopaswa kutolewa kwa usawa bila kuzingatia, jinsia ya mtu, tabaka lake katika jamii, dini yake au mfungamano wake na kundi, kaumu au lugha fulani.

Kuhusiana na hili, Debarati Guha, mweledi wa masuala ya kisiasa anaamini kuwa:

Kunyimwa Waislamu wahajiri haki ya kupata uraia wa India ni ubaguzi wa wazi unaofanywa na serikali ya New Delhi na hatua hiyo si tu kwamba, ni kinyume na katiba ya India, bali inafanyika kwa msingi wa kueneza Uhindu nchini kwa anuani ya usekulari.

Ukweli wa mambo ni kuwa, serikali ya Kihindu ya Waziri Mkuu Narendra Modi inaipuuza wazi jamiii ya Waislamu katika eneo huku ndani ya India kwenyewe ikiwa imetangaza kuhitimisha faili la muda mrefu la kesi ya Msikiti wa Babri kwa maslahi ya asasi za Kihindu zenye misimamo ya kufurutu ada ambao ulibomolewa mwaka 1992 na Wahindu wenye misimamo mikali.Serikali ya India inadai kwamba, inawapatia uraia wananchi wa mataifa ya Pakistan, Bangladesh na Afghanistan ambao kimsingi sio Wahindu na ambao katika nchi zao wanakabiliwa na adha na masaibu. Hii ni katika hali ambayo, Waislamu wa jamii ya Rohingya wa Myanmar nao wanakabiliwa na mateso, ukandamizaji na mauaji kutoka kwa wanajeshi wa nchi yao lakini macho ya serikali ya India hayawaoni Waislamu hao.

 

Tukio la kuchomwa moto msikiti wa Babri

Miongoni mwa sheria hizo ni ile ya mwezi Disemba 2019, ambapo serikali ya India ilipitisha sheria ya uhamiaji ambayo inaharakisha utoaji wa uraia kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ikiwa tu ni Wahindu au wa imani zingine, isipokuwa Waislamu. Hii ni katika hali ambayo, kupata uraia kwa mujibu wa katiba ya India ni haki inayopaswa kutolewa kwa usawa bila kuzingatia, jinsia ya mtu, tabaka lake katika jamii, dini yake au mfungamano wake na kundi, kaumu au lugha fulani.

Kuwapatia Wahindu ardhi ya msikiti wa kihistoria walioubomoa wa Babri, kufutwa mamlaka maalumu ya ndani ya kujiendeshea mambo yake liliyokuwa limepewa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India ambalo wakazi wake ni Waislamu, kubatilishwa uraia wa mamia ya maelfu ya Waislamu, kupitishwa sheria mpya ya uraia na kuwapatia uraia wa India raia wa kigeni kwa sharti la kutokuwa Waislamu, ni baadhi tu ya mlolongo wa maamuzi ya kibaguzi yaliyochukuliwa na serikali ya chama tawala cha Kihindu cha Bharatiya Janata (BJP) nchini India dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.

Waislamu nchini India wamekuwa wakikabiliwa na mateso yanayofanywa dhidi yao na Wahindu

 

Mohsen Rouhi Sefat, mtaalamu wa masuala ya kisiasa anaamini kwamba:

Tangu India ilipojipatia uhuru wake mwaka 1947 juhudi zilikuwa zimejikita kuhakikisha hakufanyiki ubaguzi wa kimadhehebu katika uandaaji wa sera za nchi. Lakini tangu Waziri Mkuu Narendra Modi ashike hatamu za uongozi nchini humo ambapo serikali yake ilifanyia marekebisho sheria ya uraia, kukawa kumewekwa jiwe la msingi la kuanzishwa kampeni kali ya ubaguzi dhidi ya Waislamu na filahi tunashuhudia utekelezwaji wa sheria hiyo.

Hii ni katika hali ambayo,  Waislamu nchini India ndio jamii ya pili kwa ukubwa nchini humo baada ya Wahindu. Kwa muktadha huo, kuipuuza jamii ya Waislamu wapatao milioni 200 nchini India sio tu kwamba, kunaonyesha kupungua kwa uvumilivu wa kidini katika nchi hiyo tangu chama tawala cha BJP kishike hatamu za uongozi nchini India 2014, bali chama hicho kimechora rasmi mstari wa wazi wa ubaguzi dhidi ya Waislamu katika jamii yenye mielekeo mingi.