WHO: Hospitali 600 zimeshambuliwa miaka miwili iliyopita
https://parstoday.ir/sw/news/world-i7897-who_hospitali_600_zimeshambuliwa_miaka_miwili_iliyopita
Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani WHO imebaini kuwa mashambulizi takriban 600 yamelenga wauguzi ulimwenguni kote mwaka 2014 na 2015 na kusababisha vifo zaidi ya 900.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2016 02:38 UTC
  • WHO: Hospitali 600 zimeshambuliwa miaka miwili iliyopita

Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani WHO imebaini kuwa mashambulizi takriban 600 yamelenga wauguzi ulimwenguni kote mwaka 2014 na 2015 na kusababisha vifo zaidi ya 900.

Utafiti huo umefanyika kwenye nchi 19 tu ambako takwimu zilikuwa zinapatikana ambapo Syria ndiyo inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na mashmbulizi zaidi ikifuatiwa na Ukanda wa Ghaza na ya tatu ni Iraq.

Rick Brennan ambaye ni mkurugenzi wa WHO wa idara ya masuala ya dharura anasema huenda moja ya matokeo ya ripoti yanayotia wasiwasi zaidi ni kwamba karibu theluthi mbili ya mashambulizi dhidi ya huduma za afya, vituo vya afya, wauguzi, magari ya wagonjwa na wagonjwa yamekuwa ni ya makusudi.”. Ikumbukwe kuwa ndege za kivita za Saudia zimeshambulia hospitali mara kadhaa katika hujuma zake zinazoendelea dhidi ya taifa la Yemen. Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imesema Saudia imeshambulia hospitali zake Yemen kwa makusudi. Aidha jeshi la Marekani pia limeshambulia hospitali mara kadhaa katika vita vya Afghanistan na kusababisha hasara kubwa. Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) ilitangaza kuwa shambulizi lililofanywa na ndege za kivita za Marekani dhidi ya hospitali ya jumuiya hiyo katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan mnamo Oktoba 3 lilifanyika kwa makusudi kwa ajili ya kuua watu na kufanya uharibifu.