Uholanzi yakataa kupiga marufuku kampeni dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i7906-uholanzi_yakataa_kupiga_marufuku_kampeni_dhidi_ya_israel
Uholanzi imekataa wito wa utawala wa kibaguzi wa Israel wa kupiga marufuku kampeni inayozidi kupanuka ya kimataifa ya kutaka walimwengu wasusie bidhaa za Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2016 03:21 UTC
  • Uholanzi yakataa kupiga marufuku kampeni dhidi ya Israel

Uholanzi imekataa wito wa utawala wa kibaguzi wa Israel wa kupiga marufuku kampeni inayozidi kupanuka ya kimataifa ya kutaka walimwengu wasusie bidhaa za Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Bert Koenders amesema nchi yake imeufahamisha utawala wa Israel kuwa watu wanaojiunga na kampeni hiyo wana uhuru wa kufanya hivyo.

Uholanzi ni nchi ya pili ya Umoja wa Ulaya kutangaza kuwa wananchi wake wana uhuru wa kujiunga na kampeni ya kimataifa ya kususia bidhaa za utawala wa Israel ijulikanayo kama BDS.

Sweden pia imesema wananchi wake wana uhuru wa kujiunga na kampeni ya kususia bidhaa za Israel na kwamba serikali haiwezi kuwazuia wanaotaka kujiunga na kampeni hiyo.

Mapema mwezi juu zaidi ya makundi 300 ya Ulaya yaliutaka Umoja wa Ulaya kuushurutisha utawala wa kibaguzi wa Israel uwajibike kuhusu ukiukaji wake wa haki za binadamu dhidi ya Wapalestina. Aidha wameutaka Umoja wa Ulaya ujiunge na kampeni ya kimataifa ya kususia bidhaa za Israel.

Kampeni ya BDS ilianzishwa mwaka 2005 na mashirka ya Palestina kwa lengo la kuwataka walimwengu wasusie bidhaa na huduma zote za utawala haramu wa Israel hadi utawala huo utakapotii sheria za kimataifa na uache kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.