EU: Mazungumzo ya Vienna yamefika katika marhala hasasi
(last modified Wed, 23 Feb 2022 02:40:36 GMT )
Feb 23, 2022 02:40 UTC
  • EU: Mazungumzo ya Vienna yamefika katika marhala hasasi

Naibu Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema mazungumzo ya Vienna yenye lengo la kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanaelekea ukingoni, na hivi sasa yako katika marhala hasasi na nyeti.

Enrique Mora amesema hayo katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kueleza kuwa: Mazungumzo ya Vienna yapo katika hatua nyeti. Tunaelekea kufika tamati baada ya miezi kumi ya majadiliano. Matokeo yake bado hayajulikani.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa EU amebainisha kuwa, bado kuna masuala nyeti yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi, na kwamba wajumbe wa pande zote wanafanya juu chini kuhakikisha kuwa natija inapatikana.

Mazungumzo ya Vienna

Duru ya nane ya mazungumzo ya Vienna kwa ajili ya kuiondolea Iran vikwazo vya kidhalimu na haramu ilianza tena tarehe 8 mwezi huu wa Februari baada ya mapumziko mafupi kwa lengo la kuchukuliwa maamuzi ya kisiasa.  

Iran inasisitiza kuwa inasubiri maamuzi ya Ulaya na Marekani kuhusiana na mazungumzo hayo ya Vienna ya kuondolewa Tehran vikwazo.

 

Tags