Russia: Marekani na washirika wake wanaunda silaha za kibaolojia nchini Ukraine
Russia imekutaja kuwepo kwa shughuli za kibaolojia nchini Ukraine kuwa ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa na kutangaza kuwa, ina nyaraka zinazothibitisha kuwepo kwa maabara 30 za kibaolojia zenye kemikali za vimelea vinavyosababisha magonjwa hatari kama tauni na kimeta kupitia ndege wanaohama kati ya Ukraine na Russia.
Moscow pia imeitahadharisha jamii ya kimataifa kuhusu hatari ya magaidi kuiba silaha hizo za kibaolojia kutoka kwenye maabara za Ukraine.
Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzya amebainisha kuwa, mpango huo wa kutengeneza silaha za kibaolojia nchini Ukraine unafadhiliwa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) na kusema: "Tumegundua ukweli wa kutisha unaoonyesha kuwa, Ukraine imekuwa ikisafisha kwa haraka athari za silaha zake za kibaolojia, na kuna uwezekano kwamba silaha hizo hatari zimeingizwa Ulaya au Russia. Nebenzya amesisitiza kuwa: "Uchambuzi wa data tulizopata unaonyesha kuwa mada na silaha hizo za kibaolojia zina uwezo wa kulenga makundi maalumu ya kikaumu."
Kufichuliwa kwa maudhui hii kunaonesha sera halisi ya Marekani ya kustawisha silaha zilizopigwa marufuku za maangamizi, ikiwa ni pamoja na silaha za kibaolojia duniani. Nyaraka zilizopatikana zinathibitisha ushirikiano wa Marekani na Ukraine katika kutengeneza silaha za kibaolojia na ukiukaji wa Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Kibaolijia na za Sumu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Zhao Lijian ameandika katika ukurasa wake rasmi wa Twitter kwamba: "Shughuli za kijeshi za silaha za kibaolojia za Marekani nchini Ukraine ni ncha tu ya mlima wa barafu. Jumla ya idadi ya maabara za kibaolojia za Marekani duniani ni 336, na ziko katika nchi 30 zinazodhibitiwa na Marekani."
Oktoba mwaka jana pia Geng Shuang, naibu mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa alionya kwamba, shughuli za kibaolojia za Marekani na washirika wake katika maabara zaidi ya 200 nje ya Marekani ni tishio kubwa kwa usalama wa Russia na China.
Katika miongo ya hivi karibuni, Marekani imezingatia sana suala la kustawisha zaidi maabara za kibaolojia, kwa kadiri kwamba mbali na kuwa na makumi ya maabara kubwa za kibaolojia ndani ya nchi, vilevile imeanzisha maabara kadhaa za kibaolojia katika sehemu mbalimbali za dunia. Katika miaka ya hivi karibuni, Russia imeeleza mara kwa mara wasiwasi wake kuhusu maabara za kibaolojia zinazofadhiliwa na Marekani nchini Ukraine na katika baadhi ya nchi za muungano wa Sovieti ya zamani.
Maafisa wa Marekani hata hivyo wamekanusha taarifa ya Russia. Msemaji wa Serikali ya Marekani, Jen Psaki amesema, madai ya Russia kuhusu ujenzi wa maabara ya silaha za kibaolojia ya Marekani nchini Ukraine ni uzushi na njama ya wazi ya kuhalalisha mashambulizi ya Russia.
Hata hivyo inatupasa kusisitiza hapa kuwa, Marekani ina historia ndefu ya kutumia silaha za kemikali na kibaolojia kuliko mchezaji mwingine yeyote katika mfumo wa kimataifa. Utumiaji mkubwa wa Marekani wa silaha za kibaolojia umethibitishwa kwa uchache katika nchi za Korea Kaskazini, Cuba na Vietnam. Kwa sasa inaonekana kuwa, Marekani si tu kwamba inaendeleza kwa nguvu zote mipango yake ya uharibifu wa kibaolojia, bali pia imehamishia sehemu kubwa ya shughuli zake za uharibifu nje ya mipaka ya nchi hiyo katika kalibu ya maabara za siri au nusu siri zilizoko katika nchi zingine kwa shabaha ya kuficha shughuli hizo haramu na zenye uharibifu.
Ripoti zilizochapishwa zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, maabara za utafiti wa kibaolojia za Marekani barani Afrika zinazofanya kazi chini ya mwavuli wa "ulinzi dhidi ya ugaidi wa kibaolojia", zimeongezeka mara kumi. Nyingi kati ya maabara hizo ziko katika nchi kama Tanzania, Nigeria, Kenya, Uganda, Liberia, Sierra Leone na Misri.
Hivi sasa baada ya Russia kufichua tena shughuli za kuzalisha siilaha za kibaolojia za Marekani nchini Ukraine, inatazamiwa kuwa jamii ya kimataifa itachukua hatua za wazi na za kuwajibika za kukabiliana na uenezaji wa silaha hizo hatari.