Russia: Hakuna Mwafrika anayepigana kwa niaba ya Moscow nchini Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i82520-russia_hakuna_mwafrika_anayepigana_kwa_niaba_ya_moscow_nchini_ukraine
Balozi wa Russia nchini Kenya amekadhibisha madai kuwa Moscow imekodisha mamluki wa Kiafrika kwenda kupigana kwa niaba yake nchini Ukraine.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 14, 2022 23:33 UTC
  • Russia: Hakuna Mwafrika anayepigana kwa niaba ya Moscow nchini Ukraine

Balozi wa Russia nchini Kenya amekadhibisha madai kuwa Moscow imekodisha mamluki wa Kiafrika kwenda kupigana kwa niaba yake nchini Ukraine.

Katika mahojiano na gazeti la Daily Nation la Kenya, Dmitry Maksimychev, Balozi wa Russia mjini Nairobi amesisitiza kuwa, hakuna raia yeyote wa nchi za Afrika anayepigana kwa niaba ya Moscow nchini Ukraine.

Amebainisha kuwa: Hakuna Mwafrika yeyote aliyesajiliwa na Russia kupigana Ukraine. Ninacho fahamu ni kuwa, kuna mamia na maelfu ya raia wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uhispania, Denmark, na Uholanzi waliokodishwa na serikali ya Kiev kuwa mamluki wao katika vita vya Unazi mamboleo, ambo wanawaua raia wa Ukraine, Waukraine-Warusi wasioiunga mkono Kiev, na wanajeshi wa Russia.

Mwanadiplomasia huyo wa Russia nchini Kenya ameeleza bayana kuwa, mamluki hao wametoka katika taasisi binafsi za kijeshi zilizoundwa na Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya, na wamekuwa wakitumiwa na Wamagharibi kufanya mauaji, kutesa na kudhalilisha mamlaka na uhuru wa kujitawala nchi tofauti katika kona mbalimbali za dunia.

Ubaguzi dhidi ya Waafrika waliokijuta kwenye mgogoro wa Ukraine

Balozi wa Russia nchini Kenya amesema vikosi vya nchi yake vitasalia Ukraine hadi pale vitakapofikia malengo makuu ya Operesheni Maalumu ya Kijeshi ya nchi hiyo, iliyoanza karibu miezi miwili iliyopita.

Hii ni katika hali ambayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, hivi sasa wanadiplomasia wa Ukraine nje ya nchi hiyo wanaendesha kampeni kubwa ya kutumia mamluki na magaidi wa kigeni katika vita dhidi ya wanajeshi wa Russia.