Putin ailaumu CIA kwa kuchoche kuuliwa waandishi wa habari wa Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i82928-putin_ailaumu_cia_kwa_kuchoche_kuuliwa_waandishi_wa_habari_wa_russia
Rais Vladimir Putin wa Russia amelilaumu shirika la kijasusi la Marekani CIA kwa kuwachochea wanajeshi wa Ukraine kuwaua waandishi wa habari wa Russia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 26, 2022 03:02 UTC
  • Putin ailaumu CIA kwa kuchoche kuuliwa waandishi wa habari wa Russia

Rais Vladimir Putin wa Russia amelilaumu shirika la kijasusi la Marekani CIA kwa kuwachochea wanajeshi wa Ukraine kuwaua waandishi wa habari wa Russia.

Putin alisema hayo jana mjini Moscow na mbali na kulilaumu shirika la kijasusi la Marekani CIA kwa kuwachochea wanajeshi wa Ukraine kuwaua waandishi wa habari wa Russia amesema kuwa, kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha kuwa mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi yakiongozwa na lile la Marekani la CIA yanafanya njama za kila namna dhidi ya Russia ikiwa ni pamoja na kuwachochea wanajeshi wa Ukraine kuwaua waandishi wa habari wa Russia ili wasifichue uongo wa propaganda za vyombo vya habari vya Magharibi.

Vile vile rais huyo wa Russia amezionya nchi za Magharibi zinazopeleka silaha zao kwa mamluki wao huko Ukraine kwa kusema, nchi za Magharibi zinachochea umgwagani wa damu nchini Ukraine.

Vita nchini Ukraine

 

Mara chungu nzima Russia imezionya nchi za Magharibi ziache kurundika silaha zao huko Ukraine ikisisitiza kuwa, huo ni uvunjaji wa wazi wa haki za binadamu kwani wanajeshi wa Ukraine wanazitumia silaha hizo kuwashambulia raia wa Kirusi wa nchi hiyo kama ambavyo pia mashirika ya kijasusi yanawachochea wanajeshi hao wa Ukraine kutumia silaha hizo kuwaua waandishi wa habari wa Russia suala ambalo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kulinda usalama wa waandishi wa habari.

Katika kipindi cha miaka iliyopita nchi za Magharibi hasa Marekani zimekuwa zikiipa serikali ya Ukraine misaada ya kila namna ya kifedha na kijeshi na hadi hivi sasa zinaendelea kufanya hivyo.