Watoto wawili wa Rais wahukumiwa kifungo jela kwa mihadarati
https://parstoday.ir/sw/news/world-i8422-watoto_wawili_wa_rais_wahukumiwa_kifungo_jela_kwa_mihadarati
Duru za habari kutoka nchini Mauritania zimetangaza habari ya kuhukumiwa kifungo jela watoto wawili wa rais wa zamani wa nchi hiyo kwa tuhuma za kufanya magendo ya mihadarati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 04, 2016 00:05 UTC
  • Watoto wawili wa Rais wahukumiwa kifungo jela kwa mihadarati

Duru za habari kutoka nchini Mauritania zimetangaza habari ya kuhukumiwa kifungo jela watoto wawili wa rais wa zamani wa nchi hiyo kwa tuhuma za kufanya magendo ya mihadarati.

Shirika la habari la France Press limeripoti habari hiyo kutoka Nouakchott na kuongeza kuwa, Sid Muhammad na Ali Sheikh, watoto wawili wa rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Khouna Ould Haidalla aliyekuwa Rais wa Mauritania kuanzia mwaka 1980 hadi 1984, wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 15 na miaka minne jela kwa utaratibu baada ya kupatikana na hatia ya kufanya magendo ya madawa ya kulevya.

Aidha mtuhumiwa mmoja anayejulikana kwa jina la Ali Hamdi Ould Abubakrin amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 11 jela na mtu wa nne anayejulikana kwa jina la Almaalum Ould Ahmad Bilal, amepewa adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela.

Duru za mahakama za Mauritania zimetangaza kuwa, watuhumiwa wengine 9 wameashiliwa huru na mahakama ya rufaa ya Nouakchott baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha.

Watu hao ni sehemu ya kundi la watuhumiwa waliotiwa mbaroni baada ya kupatikana tani 13 za mihadarati ijulikanayo kwa jina la marijuana ya India, tarehe 30 Januari mwaka huu katika fukwe za Mauritania.