Aina mpya ya Omicron yaenea nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i89338-aina_mpya_ya_omicron_yaenea_nchini_marekani
Utafiti mpya wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magojwa cha Marekani (CDC) umebaini kuwa, aina mpya ya kirusi cha corona cha Omicron, imesambaa mno nchini Marekani.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 16, 2022 04:44 UTC
  • Aina mpya ya Omicron yaenea nchini Marekani

Utafiti mpya wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magojwa cha Marekani (CDC) umebaini kuwa, aina mpya ya kirusi cha corona cha Omicron, imesambaa mno nchini Marekani.

Jarida la Hill limeripoti kuwa, data za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani zinaonesha kuwa, aina mpya za kirusi cha Omicron za BQ.1 na BQ1.1 zimeunda asilimia 5.7 ya maambukizi yote ya corona nchini Marekani katika kipindi cha wiki moja iliyopita. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kitaifa Mzio na Magonjwa na Kuambukiza ambaye pia ni mshauri wa Rais wa Marekani Joe Biden, amesema wananchi wanapaswa kuwa na tahadhari kuhusiana na spishi mpya za virusi vya corona licha ya kwamba maambukizi ya virusi hivyo yamepungua. 

Anthony Fauci amesema ana wasiwasi kwamba spishi mpya za virusi vya corona zitakuwa sugu mbele ya damu zinazotengenezwa na wanasayansi kwa ajili ya kukabiliana na virusi hivyo.

Zaidi ya Wamarekani milioni moja na elfu 90 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya corona.