Nchi 8 zatahadharisha kuhusu shughuli za kibaolojia za Marekani huko Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i89440-nchi_8_zatahadharisha_kuhusu_shughuli_za_kibaolojia_za_marekani_huko_ukraine
Nchi 8 zimetaka katika kikao cha Umoja wa Mataifa kutumiwa njia zote zilizopo ili kuweka wazi taarifa zinazohusiana na shughuli za kibaolojia zinazofanywa na jeshi la Marekani huko Ukraine.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 19, 2022 04:30 UTC
  • Nchi 8 zatahadharisha kuhusu shughuli za kibaolojia za Marekani huko Ukraine

Nchi 8 zimetaka katika kikao cha Umoja wa Mataifa kutumiwa njia zote zilizopo ili kuweka wazi taarifa zinazohusiana na shughuli za kibaolojia zinazofanywa na jeshi la Marekani huko Ukraine.

Russia Septemba mwaka huu ilitangaza kuwa ina ushahidi na nyaraka zinazothibitisha kuwa, Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imekuwa ikizidhaminia fedha zaidi ya maabara 30 za kibaolojia za Ukraine na tayari kumefanyika utafiti wa hatari sana kwa njia ya siri uliowashirikisha na kuongozwa na wataalamu mbalimbali katika uwanja huo.  

Ripoti ya leo asubuhi ya shirika la habari la IRNA la Iran imeeleza kuwa, Russia pamoja na Belarus, Venezuela, Zimbabwe, China, Cuba, Nicaragua na Syria katika kikao cha Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zimetaka kutolewa majibu kuhusu taarifa zinazohusiana na shughuli za kibaolojia za jeshi la Marekani huko Ukraine. 

Konstantin Vorontsov Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kuzuia Uenezi na Udhibiti wa Silaha katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ndiye aliyesoma taarifa ya pamoja ya nchi hizo nane. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bado kunasalia maswali yanayohusiana na shughuli za kijeshi za kibaolojia za Marekani kuhusu namna maabara hizo za kibaolojia zinavyofanya kazi huko Ukraine.  

Taarifa ya nchi hizo 8 imeongeza kuwa, bado jibu kamili halijatolewa ili kuondoa shaka iliyopo khusu shughuli hizo; na kwa sababu hiyo, ili kutatua suala hilo upande wa Russia umelazimika kuitisha mkutano wa mashauriano kujadili kifungu cha 5 cha Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Kibiolojia na Kemikali (BTWC).

Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Kibiolojia na Kemikali