Marekani yaingiwa na wahaka kufuatia maridhiano ya Syria na HAMAS
Marekani imeonya kuwa itachukua hatua zaidi za 'kumtenga' Rais Bashari al-Assad wa Syria, jambo linaloashiria kuwa Washington imeingiwa na kiwewe kufuatia hatua ya hivi karibuni ya Damascus kufikia maridhiano na Harakati ya Mapmbano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS).
Ned Price, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameeleza 'wasi wasi' wa Washington kufutia hatua ya Rais Assad kuionyooshea mkono wa maridhiano HAMAS na kudai kuwa, maridhiano hayo ni kwa madhara ya Palestina.
Afisa huyo wa Marekani ameendelea kubwabwaja kuwa, Washington itaendelea kupinga jitihada zozote za kuuhuisha utawala Assad, na haswa uungaji mkono kutoka kwa kundi ambalo Washington inadai kuwa ni la kigaidi.
Siku ya Jumatano, ujumbe wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ulikutana na kufanya mazungumzo na Rais Bashar al-Assad wa Syria, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Tarehe 21 Juni mwaka huu, duru moja ya Palestina ilitangaza kuwa, harakati ya HAMAS na serikali ya Syria zina nia ya kuanzisha tena uhusiano wao baada ya miaka 10. Uhusiano huo uliharibika baada ya kuanza mgogoro wa Syria.
Marekani imeingiwa na kiwewe kufuatia hatua hhiyo ya kufufuliwa uhusiano wa Syria na HAMAS kwa kuzingatia kuwa, ushirikiano wa pande mbili hizo huenda ukavuruga mahesabu ya Marekani ya kupora rasilimali za nchi hiyo ya Kiarabu.
Wizi na usafirishaji kimagendo mafuta ya Syria ungali unaendelea kufanywa na wanajeshi wa Marekani na wanamgambo wenye mfungamano na Washington katika ardhi ya nchi hiyo.
Tangu mwaka 2011, wakati Syria ilipolazimishwa kuingia kwenye vita vya kupambana na magaidi, mbali na Marekani kuyaunga mkono baadhi ya makundi ya magaidi, lakini pia imekuwa ikilipa kipaumbele suala la uporaji wa maliasili za nishati za nchi hiyo