Jan 16, 2023 02:26 UTC
  • Indhari ya Evo Morales kuhusu nia ya Marekani ya kufanya mapinduzi Amerika ya Latini

Evo Morales, Rais wa zamani wa Bolivia amesema kuwa, Marekani ipo katika mkondo wa kuporonmoka hasa kwa kuzingaia matukio ya hivi karibuni katika baadhi ya mataifa ya Amerika ya Latini na ni kutokana na sababu hiyo ndio maana Washington imeamua kutumia mabavu na kwamba, hivi sasa inatekeleza njama za mapinduzi katika maeneo ya Ukanda huo.

Rais huyo wa zamani wa Bolivia amesisitiza kuwa, siasa za Marekani huko Amerika ya Latini zimefeli na kugonga ukuta na kwamba, zama za Washngton za kuwa na mamlaka ya kutoa amri katika eneo hilo zimefikia ukingoni. Morales anasema: Wakati utawala fulani unapokabiliiwa na hali mbaya hutumia mabavu na wakati unapopoteza mamlaka ya kutoa amri, hukimbilia silaha na risasi. Marekani imo katika hali ya kupanga mapinduzi katika mataifa ya Amerika ya Latini baada ya kupoteza sauti na mamlaka ya kutoa amri.

Indhari ya Ivo Morales inatolewa hasa kwa kuzingatia matukio ya hivi karibuni huko Latin America hususan baada ya kushuhudiwa viongozi wa mrengo wa kushoto ambao ni wapinzani wa siasa za Marekani wakiingia madarakani.

Kwa mujibu wa Morales ni kuwa, katika miezi ya hivi kkaribuni Washington imefanya mapinduzi ya kisheria dhidi ya Cristina Kirchner, Makamu wa Rais wa Argentina na baada ya hapo ikafanya mapinduzi ya Bunge katika nchi ya Peru na hivi sasa inafanya njama za kufanya mapinduzi nchini Brazil. Evo Morales yeye mwenyewe ni mhanga wa siasa za majitaka za Marekani ambapo mwaka 2019 alilazimikka kuachia madaraka kufuatia maandamano ya wananchi na mashinikizo ya jeshi, tukio ambalo lilishabihiana na mapinduzi ambayo yaliungwa mkono na Marekani.

Kuanzia mwanzoni mwa karne ya 19 Marekani imekuwa ikilihesabu eneo la Amerika ya Latini kama uwanja wake wa kujifaragua kupitia Kanuni ya Monroe (The Monroe Doctrine). John Bolton, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani sanjari na kuashiria kanuni hiyo ambayo inalitambua wazi eneo la Amerika ya Latini kuwa uwanja wake wa kupenya, amesema, Washinghton ina haki ya kuingilia masuala ya ndani ya mataifa ya eneo hilo kwa ajili ya kufikia malengo yake ya Kanuni ya Monroe.

Ukweli wa mambo ni kuwa, hadi sasa Washington ingali inalitambua eneo la Amerika ya Latini kama lililo katika mamlaka yake na ni kwa sababu hiyo ndio maana daima imekuwa na uhasama na chuki na wakati huo huo kufanya njama za kuwaondoa madaraka viongozi na tawala za mrengo wa kushoto katika eneo hilo ambazo zinakwenda kinyume na matakwa pamoja na maslahi ya Washington. Hatua hizo za Washington zimewekwa katika ajenga zake kuu.

Wataalamu wa mambo wanaamini kuwa, utendaji huo wa Marekani unaonyesha dhati ya ubeberu iliyoko katika damu ya dola hilo vamizi. Pamoja na hayo, sera hizo za Marekani zilizopitwa na wakati zimefeli na kugonga mwamba katika mataifa kama Venezuela, Cuba, Nicaragua na Bolivia. Hivi sasa pia katika mataifa kama Mexico, Colombia, Brazil, Argentina na Chile wameingia madarakani Maraisa wa mrengo wa kushoto ambao wanafanya mambo kinyume kabisa na matakwa ya Washington.

Viongozi hao wapya wa Amerika ya Latini wanataka Marekani ikomeshe uingiliaji wake katika masuala ya ndanii ya mataifa hayo.

Katika kipindi cha baada ya viita baridi na hasa katika zama za uongozi wa Rais Donald Trump, Marekani ilifanya njama kubwa za kuwadhoofisha na kuwaondoa madarakani kwa njia ya mapinduzi wanasiasa na tawala za mrengo wa kushoto huko Amerika ya Latini hususan kupitia njia ya kushadidisha vikwazo. Hata hivyo ilifeli na kushindwa mara kadhaa kufikia malengo yake hayo machafu.

Filihali kwa mara nyingine tena wanasiasa wa mrengo wa kushoto wameingia madarakani katika baadhi ya mataifa muhimu ya Amerika ya Latini au wangali madarakani. Viongozi hao wamekuwa wakitoa himaya na kuungana mkono wao kwa wao katika kukabiliana na mashinikizo ya Marekani na vibaraka wa ndani. Licha ya kufeli siasa zake hizo, lakini Marekani ingali imeng'ang'ania sera zake hizo ambazo kimsingi hazina tena soko kutokana na mataifa ya eneo kung'amua njama za Washington za kutaka kuwa na sauti na mamlaka ya kutoa amri ambapo vikwazo na mapinduzi ni miongoni mwa nyenzo zinazotomiwa na Ikulu ya White House kwa ajili ya kufikia lengo lake. Indhari ya Evo Morales Rais wa zamani wa Bolivia bila shaka limetolewa kwa kuzingatia kadhia hii.

Tags