Jun 15, 2023 06:35 UTC
  • Rais Raisi: Muqawama, kupigania uadilifu na uhuru mataifa ya dunia kumewahamakisha mabeberu

Rais wa Jamhuri ya Kiialamu ya Iran amesema kuwa, muqawama, kupigania uadilifu na uhuru mataifa ya dunia kumewahamikisha maadui na kuwalazimisha kurudi nyuma.

Tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran, Jamhuri ya Kiislamu imekuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya nchi za eneo la Amerika ya Latini kama Nicaragua, Chuba, Venezuela na Bolivia ambazo zina historia ndefu ya kupambana na ubeberu na uistikbari duniani unaoongozwa na Marekani.

Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano wa Iran na nchi muhimu za Amerika ya Latini umezidi kustawi tena katika nyuga zote, za kisiasa, kiuchumi, kibiashara, kiviwanda, nishati, masuala ya tiba na kwenye nyuga nyinginezo.

Ni kwa sababu hiyo ndio maana, jana Jumatano, Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwa mwishoni mwa ziara yake ya kuitembelea Nicaragua, moja ya nchi muhimu za ukanda wa Amerika ya Latini, alizungumza na waandishi wa habari akiwa pamoja na rais mwenzake wa nchi hiyo na kuwaambia kwamba, kuwa na uhusiano mzuri na wa karibu na nchi huru ni katika vipaumbele vya siasa za mambo ya nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Ebrahim Raisi

 

Amesema, kama dunia itaheshimu maamuzi na matakwa ya mataifa mengine, na kama madola ya kibeberu hayatoingilia masuala ya nchi nyingine na kuwaachia wananchi wa nchi hizo kujiamulia wenyewe mambo yao, bila ya shaka hali itakuwa nzuri mno duniani.

Rais Raisi pia amesema, licha ya kuwekewa vikwazo vingi na kufanyiwa vitisho vya kupindukia, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kujiletea ustawi wa maendeleo na mafanikio makubwa katika masuala ya kisayansi, ufundi, uhandisi, masuala ya tiba, uzalishaji madawa n.k. 

Tags