Jan 23, 2023 07:14 UTC
  • Walimwengu waendelea kulaani kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu nchinii Sweden

Wananchi wa mataifa mbalimbali ya Kiislamu na yasiyo ya Kiislamu wameendelea kulaani hatua ya kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Sweden.

Maandamano ya kulaani kitendo hicho yameendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya dunia sambamba na kutaka kuchukuliwa hatua kali za kuzuia kukaririwa kitendo kama hicho huku tawala na serikali mbalimbali zikitoa taarifa ya kulaani kitendo hicho..

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iraq imeungana na mataifa mengine ya dunia kukemea na kuulaani vikali hatua ya kijeuri ya kuchomwa moto Qur'ani Tukufu huko Stockholm mji mkuu wa Sweden.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iraq imeeleza kuwa, kitendo hicho cha kujeruhi hisia za Waislamu kwa kuvunjia heshima matukufdu yake katu hakikubaliki. Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeitaka jamii ya kimataifa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuhitimisha vitendo kama hivyo.

Rasmus Paludan

 

Harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Jihadul Islami nayo imelaani hatua hiyo na kuitaja kuwa isiyo kubalika. Aidha Hizbullah ya Lebanon na Chuo Kikuu cha al-Azhar cha nchini Misri nazo katika taarifa zao tofauti zimekemea kitendo hicho.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amelaani jinai ya kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu huko Stockholm Sweden na kuitaka serikali ya Sweden kuwachukulia hatua zinazopasa wahusika wa hujuma hiyo. 

Kabla ya hapo mataifa mengine kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saudi Arabia, Kuwait, Pakistan, Jordan na Uturuki yalijoteza jana kulaani kitendo hicho.

Hii ni baada ya baada ya kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia mwenye chuki dhidi ya Uislamu wa Denmark, Rasmus Paludan, kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya ubalozi wa Uturuki nchini Sweden. 

Tags