Sanders ataka mabadiliko katika chama cha Democratic Marekani
Bernie Sanders anayewania nafasi ya kuwakilisha chama cha Demicratic katika uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani ametoa wito wa kufanyika mabadilliko ya kimsingi ndani ya chama hicho akisema kuwa kinadhibitiwa na matajiri na wafadhili.
Sanders amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na mpinzani wake, Hillary Clinton katika kufanya mageuzi ndani ya chama cha Democratic. Ameongeza kuwa anatarajia Clinton atakiongoza chama cha Democratic na kuwa chama cha kisasa na chama cha tabaka la wafanyakazi na vijana badala ya kuwa chama cha matajiri na wafadhili.
Amesema chama cha Democratic kinapaswa kuwa na ujasiri wa kupambana na Wall Street, viwanda vya madawa, mafuta na makundi mengine ya mashinikizo ambayo yanadhibiti siasa na uchumi wa wananchi wa Marekani.
Hata hivyo Sanders hakuweka wazi kama atajiengua katika kinyang'anyiro cha kugombea tiketi ya kukiwakilisha chama cha Demcratic katika uchaguzi ujao wa rais kwa maslahi ya Hillary Clinton.