Jimmy Dore: Marekani ndio gaidi mkubwa zaidi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i93674-jimmy_dore_marekani_ndio_gaidi_mkubwa_zaidi_duniani
Msanii mashuhuri wa filamu za kuchekesha wa Marekani ameitaja nchi yake kuwa ndio gaidi mkubwa zaidi duniani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 05, 2023 02:35 UTC

Msanii mashuhuri wa filamu za kuchekesha wa Marekani ameitaja nchi yake kuwa ndio gaidi mkubwa zaidi duniani.

Katika mahojiano yake na televisheni ya Fox News ya Marekani, Jimmy Dore ameitaja nchi hiyo kuwa ni gaidi, na kuishutumu Marekani kwa kuanzisha vita vingi duniani.

Dore amesema: "Katika miaka ishirini iliyopita, tulianzisha moto wa vita Asia Magharibi na sasa tunapigana vita vya wakala nchini Ukraine. Vita hivi vilizinduliwa na Marekani na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO)."

Msanii huyo wa filamu za kuchekesha wa Marekani amedokeza kuwa Washington hivi sasa inafanya mikakati ya kuanzisha vita na China na kusema kuwa, China na Russia sio maadui zao. Amesema adui wa Marekani ni viwanda vya zama za kijeshi vya Marekani yenyewe, ambavyo vimeiibia nchi hiyo mamia ya mabilioni na trilioni za dola.

Tangu kuanza vita vya Ukraine mnamo Februari 2022, Marekani imetumia zaidi ya dola bilioni 27.2 kwa ajili ya misaada ya kijeshi kwa serikali ya Ukraine.