Jumamosi, 10 Mei, 2015
Leo ni Jumamosi 12 Mfunguo Pili Dhul-Qaadah 1446 Hijria mwafaka na 10 Mei 2025 Miladia.
Miaka 279 iliyopita katika siku kama ya leo Gaspard Monge, mwanasayansi wa Ufaransa na mvumbuzi wa jiometri ya picha, alizaliwa. Alikuwa mtoto wa mfanyabiashara msafiri na alifanya kazi hadi alipokuwa na umri wa miaka kumi na sita, lakini baada ya muda aligeukia elimu. Monge alihuisha upya utafiti wa baadhi ya matawi ya jiometri, na kazi yake ilikuwa sehemu ya kuanzia ya kustawi kwa ajabu kwa uwanja huo katika karne ya 19. Mbali na hisabati, pia alikuwa na ujuzi wa kemia na aliwasaidia sana wanamapinduzi wa Ufaransa wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa kwa kutoa baruti na vilipuzi.

Siku kama ya leo miaka 196 iliyopita,alizaliwa François-Marie Raoult, mwanakemia wa Ufaransa. Baada ya kupokea shahada yake ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Paris, alipanua utafiti wake wa kielimu na hatimaye akawa mmoja wa waanzilishi wapya wa elimu za kemia na fizikia. Raoult alipendekeza nadharia ya kupunguza kiwango cha kuganda na kuinua kiwango cha mchemko ambacho kimesajiliwa kwa jina lake mwenyewe. Sheria za Raoult pia hutumiwa kuamua takriban molekuli ya vipengele.

Katika siku kama ya leo miaka 114 iliyopita, bodi ya ushauri wa kifedha ikiongozwa na Mmarekani Morgan Shuster iliwasili Tehran ili kurekebisha masuala ya kifedha ya Iran. Kufuatia kibali cha bunge cha kuajiri washauri wa nchi za kigeni kwa ajili ya kuboresha hali ya uchumi wa nchi, serikali ya Iran, kufuatia makubaliano na Marekani, iliukaribisha ujumbe wa washauri wa masuala ya fedha nchini Iran ili kufanya mageuzi ya masuala ya fedha, na siku hii, ujumbe ulioongozwa na Morgan Shuster uliwasili nchini Iran. Bunge la Kitaifa likiwa na imani na nia njema ya Shuster na washirika wake, liliwapa mamlaka kamili ya shughuli yoyote ya kurekebisha masuala ya kifedha ya Iran, lakini hatua hii ya Iran iliigharimu serikali ya Urusi, na Warusi waliazimia kumfukuza Shuster na manaibu wake. Kwa hivyo, chini ya kisingizio cha uwongo, waliipa serikali ya Iran amri ya kumfukuza Shuster, hatua ambayo ilikabiliwa na upinzani kutoka kwa bunge. Wakati huo huo, vikosi vya Urusi pia vilishambulia miji ya Azerbaijan, haswa Tabriz, na kufanya mauaji na uporaji.

Miaka 85 iliyopita, jeshi la Ujerumani la Nazi lilivamia Ubelgiji, Uholanzi, na Luxemburg. Vita vya Pili vya Dunia vilipoenea kote Ulaya, Hitler alipanga kuivamia Norway na kujitayarisha kwa ajili hiyo mnamo Aprili 1940, lakini kuwepo kwa meli za Uingereza katika bandari za Norway kulifanya jambo hilo kuwa gumu. Norway ilikabiliana na Wajerumani hadi mwishoni mwa Aprili kwa msaada wa meli za vita vya Uingereza, lakini kuibuka kwa upinzani wa ndani dhidi ya kuendelea kwa vita na kuundwa kwa serikali inayounga mkono Ujerumani huko Norway kulivunja kusimama kidete Norway, na kwa kuondoka kwa familia ya kifalme ya Norway na wanachama wa serikali yake kutoka nchini, vikosi vya Uingereza pia viliondoka katika bandari za Norway 03, 12 na 14 Mei. Mara tu baada ya majeshi ya Uingereza kuondoka Norway, Hitler aliamuru mashambulizi dhidi ya kambi ya Magharibi.

Katika siku kama ya leo miaka 50 iliyopita, kundi linalopigania uhuru wa Sahara Magharibi liliasisi Harakati ya Kupigania Uhuru ya Polisario. Harakati hiyo ilikaribishwa na wakazi wa eneo hilo na ikaanzisha mapambano dhidi ya wakoloni wa Kihispania hadi wakoloni hao walipoondoka Sahara mwaka 1975. Hata hivyo serikali ya Uhispania ilikabidhi mamlaka ya eneo hilo kwa serikali za Morocco na Mauritania. Mauritania ililazimika kuondoka Sahara Magharibi kutokana na mapambano makali ya Polisario na hali mbaya ya ndani ya nchi hiyo. Morocco iliendelea kukabiliana na wapigania uhuru wa Polisario hadi mwaka 1991 ambapo mapigano kati ya pande hizo mbili yalisitishwa chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa. Eneo hilo lingali linakaliwa na Morocco.

Siku kama ya leo miaka 45 iliyopita, nembo ya mwisho ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliidhinishwa na Imam Khomeini. Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, iliamuliwa kutambulishwe nembo kama ishara na alama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Ira ambayo itakuwa ikibainisha moyo wa kidini na Uislamu wa taifa la Kiislamu la Iran. Kwa hiyo, baada ya Baraza la Mapinduzi kutaka kutayarishwa nembo, kuliwasilishwa nembo nyingi kwenye baraza hilo, na hatimaye moja kati ya hizo ilikubaliwa. Nembo hii iko katika umbo la duala la miezi minne na nguzo ya kati, inayowakilisha neno takatifu "Allah" na wakati huo huo kuunda neno "La ilaha illallah".
