Hizbullah yatwanga ngome za Israel kwa makombora na droni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i137312-hizbullah_yatwanga_ngome_za_israel_kwa_makombora_na_droni
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa mapema leo ikisema kwamba imeshambulia ngome za utawala haramu wa Israel kaskazini na katikati mwa ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).
(last modified 2026-03-12T04:45:42+00:00 )
Mar 12, 2026 04:45 UTC
  • Hizbullah yatwanga ngome za Israel kwa makombora
    Hizbullah yatwanga ngome za Israel kwa makombora

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa mapema leo ikisema kwamba imeshambulia ngome za utawala haramu wa Israel kaskazini na katikati mwa ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).

Taarifa iliyotolewa na Hizbullah imesema, kambi ya Beit Lid, kituo cha kutoa mafunzo ya kijeshi, kambi ya Unit 8200 iliyoko katika viunga vya Tel Aviv na kitongoji cha jeshi la Israel cha Naharia ni miongoni mwa maeneo yaliyolengwa kwa makombora ya kisasa na ndege za kujilipua zisizo na rubani za harakati hiyo.

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeongeza kuwa, mkusanyiko wa wanajeshi wa Israel katika kambi mpya ya Markaba na kituo cha Kamandi ya Udhibiti na Operesheni za Anga cha Merun huko kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina pia vimeshambuliwa mapema leo Alkhamisi kwa makombora na ndege zisizo na rubani za wapiganaji wa Hizbullah.