Jumanne, tarehe 13 Mei, 2025
Leo ni Jumanne tarehe 15 Dhulqaada 1446 Hijria inayosadifiana na tarehe 13 Mei mwaka 2025.
Siku kama ya leo miaka 946 iliyopita, alifariki dunia Ibn Fakhir, msomi na mtaalamu mkubwa wa lugha wa Kiislamu mjini Baghdad.
Akiwa kijana, Ibn Fakhir alifanya safari huko Makkah na Yemen na kukutana na maulama wakubwa wa zama hizo, ambapo alitokea kuwa alimu mkubwa wa lugha na Hadithi.
Miongoni mwa athari za Ibn Fakhir ni pamoja na kitabu kinachoitwa ‘Jawabul-Masaail.’

Siku kama ya leo miaka 312 iliyopita alizaliwa mjini Paris, Alexis Cloude Clairaut mwanahesabati mashuhuri wa Ufaransa.
Alikuwa na hamu kubwa na somo la hesabati ambapo akiwa na umri mdogo wa miaka 18 alifanikiwa kujiunga na Chuo cha Sayansi cha Ufaransa.
Clairaut alipata umashuhuri mkubwa duniani kutokana na utafiti makini aliofanya katika nyanya tofauti za sayansi. Msomi huyo aliaga dunia mwaka 1765.

Katika siku kama ya leo miaka 179 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 13 Mei 1846, Kongresi ya marekani ilipasosha tangazo la vita dhidi ya Mexico.
Vita hivyo vilivyochukua muda wa miaka miwili, vilitokea baada ya Marekani kudai kwamba wahajiri wa nchi hiyo wanateswa nchini Mexico. Hata hivyo ukweli ni kuwa, Marekani ilianzisha mashambulizi hayo kwa lengo la kuyatwaa baadhi ya maeneo ya Mexico hususan eneo la Texas.
Katika vita hivyo, Marekani iliyakalia kwa mabavu majimbo ya Texas, California, Nevada, Utah, Arizona na New Mexico.

Katika siku kama ya leo miaka 118 iliyopita alizaliwa Bi Daphne du Maurier mwandishi wa riwaya, wasifu na thamthiliya wa Kiingereza.
Maurier alizaliwa katika familia ya wanasanaa na iliyokuwa pia na wanafasihi. Ni kutokana na kukulia katika mazingira kama hayo, ndipo Bi Daphne du Maurier akafanikiwa kukuza kipaji chake katika uwanja wa uandishi.
Miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri ni Scapegoat na Rebecca. Mwandishi huyo aliaga dunia mwaka 1889.
