Aug 05, 2016 09:04 UTC
  • Maswali Yetu na Majibu ya Thaqalain (133)

Assalaam aleikum wapenzi wasikilizaji wa idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu inayokutangazieni kutoka mjini Tehran. Katika Kipindi hiki bado tunaendelea kujibu maswali yanayohusiana na Uimamu ambapo swali letu katika kipindi hiki ni, je, ni kwa nini katika Hadithi ya Thaqalain.

Mtume Mtukufu (saw) alisisitiza kwamba wokovu wa Waislamu unapatikana tu katika kushikamana kwao kikamilifu na kwa pamoja na Qur’ani Tuku pamoja na kizazi chake kitoharifu (as) kwa kusema: ‘Na iwapo mtashikamana navyo sawasawa hamtapotea kamwe baada yangu.’? Ni kwa nini hakutosheka kwa kuwataka washikamane na Qur’ani tu ambayo ndio mwongozo mkuu wa Waislamu? Kuwen pamoja nasi hadi mwisho wa kipindi ili tupate kujua jibu la swali hili, karibuni.

*********

Ndugu wasikilizaji, tunaporejea na kuzingatia kwa makini kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu tanapata kwa mba kinasema kwa uwazi mkubwa na katika sehemu nyingi kwamba miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kwamba aliwajaaliwa wanadamu merejeo na watu maasumu ambao hawatendi dhambi ambao huwasaidia katika kufahamu vyema na kwa njia sahihi maana ya kitabu hicho kitukufu pamoja na hakika muhimu zilizomo kwenye kitabu hicho, hakika ambazo hazifahamika ila kupitia watu watoharifu na watukufu. Wema hao huwaongoza kwenye njia nyoofu na hivyo kuwazuia kuongozwa na waovu na wapotoshaji ambao hufuata mambo yasiyoeleweka wazi na moja kw amoja kwenye kitabu hicho kwa lengo la kuzua fitina miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu. Na bwana wa watu wema hao si mwingine bali ni Mtume Mtukufu (saw) na baada yake Maimamu wotoharifu (as) ambao Mwenyzi Mungu mwenyewe amethibitisha isma na utakasifu wao katika aya ya Tat’hir na aya nyingine za Qur’aniTukufu. Mwenyezi Mungu anasema katika aya mbili za 43 na 44 za Surat an-Nahl: ‘