Jan 19, 2026 02:57 UTC
  • Jumatatu, 19 Januari, 2026

Leo ni Jumatatu 29 Rajab 1447 Hijria mwafaka na 19 Januari 2026.

Siku kama ya leo, miaka 1171 iliyopita, alifariki dunia Abdullah bin Muslim Dinavari, maarufu kwa jina la Ibn Qutaybah akiwa na umri wa miaka 63.

Ibn Qutayba alizaliwa huko Kufa, Iraq na kushika hatamu za ukadhi huko mjini Dinavar, magharibi mwa Iran. Alitabahari katika Qur’ani, Hadithi, mashairi na fasihi.

Alimu huyo aliandiandika vitabu mbalimbali katika elimu za Kiislamu maarufu zaidi vikiwa ni “Ta’awiilu Mushkili-Qur’ani”, “Tafsiru Gharibul-Qur’an”, “Uyunul-Akhbar”, “Maani ash-Shi’ir” na “Gharibul- Hadith.”   

Siku kama hii ya leo miaka 290 iliyopita alizaliwa mvumbuzi na mhandisi wa Kiingereza James Watt.

Msomi huyo alipendelea na kuvutiwa mno na utafiti kuhusu masuala ya kisayansi. Katika utafiti wake Watt alifanikiwa kuvumbua nishati ya mvuke na kuzusha mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda hususan usafirishaji wa nchi kavu na baharini.

Miaka 228 iliyopita inayosadifiana na siku hi ya leo, alizaliwa Auguste Comte mwanafalsafa, mwanahisabati wa Kifaransa na mtaalamu wa falsafa umbile au positivism kwa kimombo.

Comte alifikia daraja ya uhadhiri katika hisabati akiwa na umri wa miaka 18 tu. Vitabu mashuhuri vya mwanafalsafa huyo wa Kifaransa ni Auguste Comte and positivism na Early Political Writings. Comte aliaga dunia mwaka 1517.

Siku kama ya leo miaka 47 iliyopita, wananchi Waislamu wa Iran wenye imani na umoja walifanya maandamano makubwa kupinga mabaki yaliyosalia ya utawala wa kifalme Shah, yaani serikali ya Shapur Bakhtiyar. 

Waandamanaji hao walitaka serikali hiyo ya kifalme itangazwe kuwa si halali, na pia kung'olewa utawala wa Shah na badala yale kuundwa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran. Siku hiyo Imam Khomeini MA akiwa mjini Paris alitoa ujumbe wa maandishi kwa wananchi wa Iran akisema kama tunavyonukuu: "Kwa uwezo wake Mola hivi karibuni nitaungana nanyi ili niweze kuwatumikia na kushirikiana bega kwa bega na matabaka yote ya wananchi kuelekea katika njia ya kujitawala na kuwa huru Iran." Mwisho wa kunukuu.   

Katika siku kama ya leo miaka 16 iliyopita, Abdul Rauf Mahmoud al-Mabhuh, mmoja wa makamanda waandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) aliuawa shahidi huko Dubai, katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mabhouh aliuawa na makachero wa Shirika la Ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel walioingia nchini Imarati wakitumia pasipoti bandia. Mabhuh alizaliwa katika familia iliyoshikamana na dini katika kambi ya Jabalia katika Ukanda wa Gaza, Palestina. Shahidi Mahmoud al-Mabhuh ni miongoni mwa waasisi wa Brigedi ya Izzudeen al-Qassam tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Baada ya kupita miezi kadhaa, Israel ilitangaza wazi kwamba, ilihusika na jinai ya kumuua Mabhuh.

Na siku ya leo tarehe 29 Dei inajulikana nchini Iran kwa jina la "Siku Taifa ya Gaza".

Siku hii ni kumbukumbu ya kumalizika vita vya siku 22 vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza ambapo vita hivyo vilifikia tamati kwa ushindi wa muqawama na mapambano ya Kiislamu huko Gaza.

Kutokana na vyombo vya Magharibi kuficha jinai za utawala haramu wa Israel na kwa upande mwingine kutokana na hamasa kubwa iliyooonyeshwa na wananchi madhulumu wa Gaza katika kutetea ardhi zao, siku hii imepewa jina la "Siku ya Kitaifa ya Gaza.