Sep 05, 2016 08:51 UTC
  • Maafa ya Mina (4)

Ni Mahujaji wa kiume tu ndio wanaoruihusiwa kuingia kwa masaa machache tu katika makaburi matakatifu ya Baqee. Kusimama na kuomba dua pembeni ya makaburi hayo ni marufuku ma marufuku hiyo ni kali zaidi kwa wale wanaotaka kusimama kando ya makaburi yaliyoharibiwa ya Maimamu Watukufu wa Nyumba ya Mtume (saw) na huandamana na vitisho na hofu kutoka kwa Mawahhabi.

Kwa hakika nchini Saudi hakuna uhuru wa kuabudu na kimsingi Mawahhabi ndio pekee wanaoruhusiwa kuhubiri na kueneza itikadi zao potovu katika eeo hilo. Katika kipindi kilichopita na baada ya kukuelezeeni kwa muhtasari matukio mawili muhimu yaliyojiri katika msimu wa Hija mwaka uliopita yaani ya kuanguka winchi au jina jingine kreni kweye Masjudul Haram na maafa ya kusikitisha ya Mia, tulikusimulieni kisa cha Hujaji mmoja wa Kiirani kwa jina la Muhammad ambaye alibahatika kuzuru Nyumba ya Mwenyezi Mugu na kushuhudia kwa karibu tukio hilo la kusikitisha. Tutaendelea kuzugumzia kisa hicho katika kipindi chetu cha leo, karibuni.

Anasema: 'Tulifika Madina ambao ni mji wa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu. Sote tulikuwa na hamu kubwa ya kuuzuru msikiti huo, Katika uwanja wa msikiti huo mwanazuoni aliyekuwa akiongoza msafara wetu alikuwa akiwafafanulia Mahujai historia fupi, sifa na fadhila za Masjidu an-Nabii. Punde si punde maafisa wa Saudia walifika ghafla mahala hapo na kututawanya. Haikufahamika mara moja ni kwa nini maafisa hao walichukua hatua hiyo ya kututawanya na kumzuia mwanazuoni huyo kuwaelezea mahujajio historia ya msikiti huo mtukufu. Katika siku zilizofuata na tukiwa katika hali ya kuyatembelea maeneo matakatifu, ya kihistoria na kidini pembeni ya mji huo wa Madina, maafisa hao walichukua hatua kama hiyohiyo ya kiuadui dhidi ya Mahujaji na kuwazuia kabisa kutekeleza ibada zao kama walivyokuwa wameazimia kufanya.Walikuwa wakiwasumbuasumbua Mahujaji na hivyo kuyafanya mazingira ya mji wa Madina kuwa ya kipolisi moja kwa moja.

Masjidu an-Nabii

Hata wakiwa ndani ya msikiti wenyewe wa Mtume (saw) maafisa usalama hao wa Saudia hawakuwaruhusu Mahujaji kutekeleza ibada zao kwa uhuru na utulivu. Kwa kutumia visingizio tofauti walikuwa wakiwakera na kuwabughudhi Mahujai ambao kwa miaka mingi walikuwa na matumaini makubwa ya kuweza kufika mahala hapo patakatifu kwa lengo la kumzuru Mtume wao Mtukufu, na kutoruhusu watekeleze ibada zao kwa utulivu na unyenyekevu.Maafisa wa Aal Soud walikuwa wakiwazuia Mahujaji kufika karibu na kugusa kaburi la Mtume na hivyo kuwalazimu kuomba dua na kumtumia salamu wakiwa wamesimama mbali na kaburi hilo. Ukandamizaji na dhulma hiyo ya maafisa wa Saudia ni kubwa zaidi kwa wale Mahujaji wanaotaka kuzuru makaburi ya Baqee. Wake, idadi kadhaa ya watoto, mmoja wa ami na binamu wawili wa Mtume Mtukufu (saw) pamoja na watukufu wengine wengi katika historia ya Kiislamu wamezikwa katika makaburi hayo. Vilevile Maimamu wa Nyumba Tukufu ya Mtume (saw) wamezikwa kwenye makaburi hayo ambapo kufikia mwaka 1926 haram zao zilikuwa zimejengwa kweye makaburi hayo. Lakii mwaka huohuo haram hizo zote zilivunjwa na kubomolewa kutokana na itikadi na fikra potovu za Mawahabi.

Makaburi ya Baqee kabla ya kuharibiwa na Mawahhabi

Kama tulivyosema mwanzoni, ni Mahujaji wa kiume tu ndio waaoruhusiwa kuingia kwenye makaburi hayo tena kwa masaa machache tu. Kusimama na kuomba dua pembeni ya makaburi hayo ni jambo lililopigwa marufuku na Mawahhabi na marufuku hiyo inatekelezwa vikali katika makaburi ya Maimamu wa Kishia wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (saw), marufuku ambayo huandamana na vitisho na onyo kali. Kwa hakika nchini Saudi hakuna uhuru wa kuabudu na kimsingi ni Mawahhabi tu ndio wanaoruhusiwa kuhubiri na kueneza itikadi yao potovu.

Makaburi ya Baqee

Baada ya siku kadhaa za kuwa kwenye mji mtakatifu wa Madina na kuondoka huko kwa kumbukumbu mbaya ya usumbufu wa Wasaudia katika kuwazuia Mahujaji kuzuru kaburi Tukufu la Mtume (saw) na mawalii wengine wa Mwenyezi Mungu pamoja na maeneo ya kihistoria na kidini katika mji huo tuliondoka huko kuelekea mji mwingine mtakatifu wa Makka. Baada ya kufika kwenye mji huo ambao umetajwa na Mwenyezi Mungu mweyewe katika Qur'ani Tukufu kuwa ni mji wa amani, tulijitayarisha kuelekea katika msikiti mtakatifu wa Masjidul Haram. Tukiwa pamoja na Mahujaji wengine wa msafara wetu tulielekea kwenye msikiti huo wa al-Kaaba ambao ni msikiti mtakatifu zaidi wa Waislamu duniani huku tukiwa na hamu na matumaini makubwa ya kufanya ibada zetu bila kusumbuliwa na mtu yeyote. Katika hatua za mwanzo za kuingia katika msikiti huo ambao ni Nyumba ya Mwenyezi Mungu kila mmoja wetu alishangazwa na adhama na utakatifu wa msikiti huo. Lakini baada ya muda, mazingatio yetu ya umaanawi wa msikiti huo ulivurugwa na majengo marefu ambayo yamejengwa na Wasaudia pembeni ya msikiti huo mtakatifu, majengo ambayo hakuna anayelewa lengo hasa la kujengwa majengo kama hayo pembeni na karibu kabisa na msikiti huo mtakatifu ambacho ni kibla cha Waislamu wote duniani.

Al-Kaaba imezingirwa na minara na majengo marefu

Baada ya kufanya tawafu, kuswali na kuomba dua tulianza kurejea hotelini. Hatukuwa tumeenda mbali kutoka msikitini hapo ambapo ghafla tulisikia sauti kubwa na ya kutisha ikitokea upande wa msikiti huo.

Kuanguka winchi kwenye Masjidul Haram

Sauti hiyo ilikuwa inatoka ndani ya Masjidul Haram. Watu wote walikimbia kwa hofu kuelekea kwenye msikiti huo ambapo walishagazwa mno na jambo waliloliona. Winchi kubwa na nzito ambayo ilikuwa juu ya msikiti  upande wa mashariki wa msikiti ilikuwa imeanguka ndani ya msikiti huo na kuwaponda Mahujai waliokuwa humo wakitekeleza ibada zao. Tukio hilo lilikuwa la kutisha sana ambapo baadhi ya Mahujaji walipodwa na wengine kukatwa viugo vyao ikiwemo mikono na miguu. Bila kupoteza wakati tulifanya haraka kwenda kuwaokoa Mahujaji waliokuwa wamenaswa kwenye ajali hiyo lakini hatukupewa fursa ya kufaya hivyo. Askari usalama wa Saudia waliwafukuza Mahujaji wote waliokuwa msikitini humo na wala hawakutoa fursa ya kupigwa picha wahanga wa tukio hilo. Nafsi zetu zilisumbuliwa na tukio hilo chungu na la kutisha kwa siku kadhaa. Baadaye utawala wa Saudia ulitangaza kuwa ni watu 107 tu ndio waliopoteza maisha yao katika tukio hilo na idadi zaidi ya mara mbili ya hao kuwa walijeruhiwa. Kama kawaida watawala wa Saudia walifunika uzembe na upuuzaji wao kuhusiana na tukio hilo na kudai kwamba ima ni upepo mkali ndio uliosababisha maafa hayo au kwamba maafa hayo makubwa na ya kutisha yalitokana na mapenzi ya Mweyezi Mungu!

Masjidul Haram baada ya kuanguka winchi

Kwa maelezo zaidi kuhusu Maafa ya Mina: http://kiswahili.irib.ir/habari/mina

Kwa maelezo zaidi kuhusu makala za Hija: http://kiswahili.irib.ir/uislamu/hija

Tags