Jumamosi, 28 Januari, 2017
Leo ni Jumamosi tarehe 29 Mfunguo Saba Rabiu Thani 1438 Hijria mwafaka na tarehe 28 Januari mwaka 2017 Miladia.
Miaka 756 iliyopita katika siku kama ya leo, alizaliwa Muhammad bin Ahmad Dhihni mwenye lakabu ya Shamsuddin mtaalmu wa elimu ya hadithi na mwanahistoria mashuhuri. Alikuwa na mapenzi makubwa ya kukusabnya hadithi. Shamsuddin akiwa na lengo la kujikamisha zaidi katika elimu hiyo alifanya safari katika maeneo mbalimbali na kupata fursa ya kusikia hadithi kutoka kwa wanazuoni mbalimbali. Alimu huyo hakuwa nyuma pia katika utunzi wa vitabu. Al-Kashif, Tabaqat al-Quraa, al-Muujam al-Saqhir na al-Muujam al-Kabir ni baadhi tu ya vitabu vyake mashuhuri.**
Siku kama ya leo miaka 75 iliyopita katika siku kama ya leo, baada ya hujuma na uvamizi wa vikosi vya Uingereza na Umoja wa Kisovieti kwa Iran kulitiwa saini mkataba wa pande tatu baina ya nchi hizo. Kwa mujibu wa mkataba huo, serikali ya muda ya Iran ililalizimika kukubali kukabidhi njia na nyenzo za mawasiliano ya ardhini, angani na baharini kwa nchi waitifaki. Mkabala na hatua hiyo, Uingereza na Umoja wa Kisovieti ziliitambua rasmi ardhi yote ya Iran.***
Miaka 51 iliyopita, Muhammad bin Abdullah bin Bahlul maarufu kwa jina la Sheibani aliaga dunia. Alikuwa mashuhuri katika elimu ya hadithi. Alimu huyo alikuwa na asili ya mji wa Kufa katika Iraq ya leo. Alifanya safari katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kwenda kusikiliza hadithi na ana vitabu katika Nyanja mbalimbali. ***
Na miaka 38 iliyopita katika siku kama ya leo sawa na tarehe 9 Bahman mwaka 1357 kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani, watu wengi wa mji wa Tehran walielekea katika msikiti wa chuo Kikuu cha Tehran, baada ya wanaharakati wa kidini kukusanyika katika chuo hicho wakipinga hatua ya utawala wa Shah ya kumzuia Imam Khomeini (M.A) asirejee hapa nchini. Watu waliandamana katika miji mingine ya Iran kupinga hatua hiyo, na kutaka kupinduliwa utawala wa kidhulma wa Shah na kurejea Imam Khomeini (M.A) hapa nchini. Siku hiyo wanajeshi wa utawala wa Shah kwa mara nyingine waliwashambulia wananchi na kujeruhi na kuua shahidi Waislamu wengi miongoni mwao. ***