Jumamosi, 10 Machi, 2018
Leo ni Jumamosi tarehe 21 Mfunguo Tisa Jamadi Thani 1439 Hijria mwafaka na tarehe 10 Machi 2018 Miladia.
Tarehe 10 Machi miaka 142 iliyopita, mvumbuzi wa Kimarekani Alexander Graham Bell alivumbua simu na siku hiyo hiyo akafanya mazungumzo ya kwanza ya majaribio ya simu na msaidizi wake Thomas Watson. Uvumbuzi huo wa simu ulileta mabadiliko makubwa katika vyombo vya mawasiliano. Bell alifaidika na uzoefu na majaribio ya wahakiki na wavumbizi wengine katika kutengeneza chombo hicho cha mawasiliano ya haraka. Baada ya hapo chombo cha simu kiliboreshwa na kufikia kiwango cha sasa kwa kukamilishwa kazi iliyofanywa na Alexander Graham Bell. ***
Siku kama ya leo miaka 122 iliyopita, Sayyid Jamaluddin Asadabadi mwanazuoni na mmoja wa viongozi wa mapambano dhidi ya ukoloni wa kimaitaifa dhidi ya Waislamu aliuawa. Sayyid Jamaluddin alizaliwa huko Asadabad magharibi mwa Iran na kupata elimu katika taalamu za falsafa, nujumu na historia. Mbali na kufahamu lugha za Kiarabu, Kifarsi na Kituruki, Sayyid Jamaluddin Asadabadi alikuwa mtaalamu pia katika lugha za Kiingereza, Kifaransa na Kirusi. ***
Na katika siku kama ya leo miaka 73 iliyopita, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia ndege za kivita za Marekani zilifanya mashambulizi makubwa dhidi ya mji mkuu wa Japan, Tokyo. Mashambulizi hayo makubwa yalishirikisha mamia ya ndege kubwa za kurusha mabomu za Marekani zilizomimina mabomu kwa mara kadhaa katika mji mkuu wa Japan. Mamia wa raia wa nchi hiyo waliuawa katika mashambulizi hayo. ***