Dec 07, 2018 20:52 UTC
  • Jumamosi, 8 Disemba, 2018

Leo ni Jumamosi tarehe 30 Mfunguo Sita, Rabiul Awwal 1440 Hijria mwafaka na tarehe 8 Disemba 2018.

Siku kama ya leo miaka 150 iliyopita, ulianguka utawala wa Washugani au kwa jina jingine watawala wa kijeshi huko Japan. Kuanguka kwa utawala huo kulipelekea kuanza kwa marekebisho ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni nchini humo. Washugani walikuwa moja kati ya makumi ya silsila zenye nguvu huko Japan, walioanzisha utawala wao wa kidikteta tangu karne ya 12 Miladia. ***

Mtawala wa zamani wa Japan

 

Katika siku kama ya leo miaka 115 aliaga dunia Herbert Spencer mwanafikra na mwanafilosofia wa Kiingereza. Spencer alizaliwa mwaka 1820 Miladia na kujifunza elimu mbalimbali kutoka kwa baba yake. Aidha alijiongezea ujuzi wa kielimu kutokana na juhudi zake za kupenda kutalii mambo. Herbert Spencer aliamini kuwa, mtu anaweza kujipatia elimu kwa kushuhudia na kupata uzoefu. ***

Herbert Spencer

 

Miaka 104 iliyopita katika siku kama ya leo, yalijiri mapigano ya baharini ya Falklands pambizoni mwa visiwa vya Falklands katika bahari ya Atlantic kati ya Uingereza na Ujerumani. Vikosi vya wanamaji vya Ujerumani vilipigwa vibaya na vile vya Uingereza na kupelekea visiwa hivyo kwa mara nyingine tena kuwa chini ya himaya ya Waingereza. ***

Falklands

 

Siku kama ya leo miaka 69 iliyopita, Chian Kai-shek kiongozi wa wapigania uhuru wa China alikimbilia Taiwan akiwa na wafuasi wake wengi baada ya kushindwa na wapiganaji wa chama cha Kikomonisti chini ya uongozi wa Mao Tse Tung na kuunda serikali ya kitaifa ya Uchina. Uungaji mkono wa Marekani kwa kiongozi huyo wakati huo ulipelekea Taiwan kujitenga na Uchina na kiti cha nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kikapatiwa Taiwan. ***

Chian Kai-shek

 

Na katika siku kama ya leo miaka 18  iliyopita sawa na tarehe 17 Azar 1378 Hijria Shamsia aliaga dunia Husseini Makki mwanasiasa, mwanahistoria na mwandishi wa zama hizi wa Iran. Hussein Makki alizaliwa mwaka 1290 Hijria Shamsia. Baada ya kukamilisha masomo ya utangulizi alielekea katika mji wa Tehran na kuanza kufanya kazi serikalini. Baada ya mwaka 1320 Hijria Shamsia kupatina anga ya wazi ya kisiasa alianza rasmi harakati zake katika magazeti. Maandishi ya Husseini Makki ya kihistoria, kiutafiti na kifasihi yalikuwa sehemu muhimu ya makala katika magezeti mashuhuri ya Tehran zama hizo. Kujiunga kwake na Chama cha Iran na Chama cha Demokrasi cha Iran ndio uliokuwa mwanzo wa safari yake ya kuelekea katika harakati za kisiasa ambapo aliwahi kushika wadhifa wa Bunge katika duru tatu mtawalia. ***

Husseini Makki