Dec 12, 2018 23:03 UTC
  • Alkhamisi tarehe 13 Disemba 2018

Leio ni Alkhamisi tarehe 5 Rabiuthani 1440 Hijria, sawa na Disemba 13 mwaka 2018.

Katika siku kama ya leo miaka 15 iliyopita, Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa Iraq alitiwa mbaroni akiwa katika maficho yake karibu na Tikrit huko kaskazini mwa Baghdad. Saddam alijificha katika eneo hilo baada ya Iraq kuvamiwa na majeshi ya Marekani na Uingereza mwezi Machi 2003. Kutiwa nguvuni dikteta huyo wa Iraq aliyemwaga damu za raia wengi wa nchi hiyo kuliwafurahisha sana Wairaqi na nchi kama vile Iran na Kuwait ambazo zimepatwa na maafa makubwa kutokana na dhulma za Saddam Hussein dhidi ya nchi hizo. Katika upande mwingine, pamoja na kuwa walimwengu walikuwa wakisubiri kwa hamu kusikia matamshi ya dikteta huyo kuhusu jinai zilizotendwa na utawala wake nchini Iraq, Marekani ilimweka dikteta huyo chini ya uangalizi wake baada ya kumtia nguvuni lengo likiwa ni kuzuia kufichuliwa ushirikiano wa karibu uliokuwapo kati ya Saddam na nchi za Magharibi hususan ikulu ya rais wa Marekani, White House.

Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa Iraq

Katika siku kama ya leo miaka 55 iliyopita, Shaikh Mahmood Shaltoot Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar na Mufti Mkuu wa Misri aliaga dunia. Mwanazuoni huyu mkubwa wa Misri alizaliwa mwaka 1892 Miladia nchini Misri. Akiwa na umri wa miaka 14 alianza masomo ya shule ya upili katika Chuo cha Kidini cha Alexandria kilichokuwa tai la Al Azhar. Alipata chetu cha chuo kikuu mwaka 1918 na kuanza kufunza katika chuo hicho hicho na kisha hatimaya akahamia chuo kikuu cha al Azhar mwaka 1927. Alizidi kupanda chei kieleimu na kuteuliwa kuwa mwanachama wa baraza la Fatwa chuoni hapo. Mwaka 1958 aliteuliwa kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar ambapo alitoa huduma kubwa. Kati ya hatua muhimu alizochukua Sheikh Shaltut katika kipindi cha uongozi wake ni hitihada za kuleta umoja na ukuruba wa madhehebu za Kiislamu. Baada ya kuandikiana barua kadhaa na Ayatulahil Udhma Borujerdi, marjaa mkubwa wa Kishia, Sheikh Shaltut alitambua rasmi Madhehebu ya Shia Ithnaashari. Aliamurhisha Madhehebu ya Shia yafunzwe katika Chuo Kikuu cha Al Azhar sawa na madhehebu zingie za Kiislamu. Aidha alitoa fatwa mashuhuri nakusema kuwa inajuzu kwa Mwislamu atakaye,  kufuata Madhehebu ya Shia Jaafariya. Sheikh Shaltut aliaga dunia mwaka 1963 akiwa na umri wa miaka 72.

Shaikh Mahmood Shaltoot

Katika siku kama ya leo miaka 93 iliyopita, Majlisi ya Waasisi nchini Iran ambayo iliundwa kwa ajili ya kuhamisha mfumo wa kisultani kutoka silsila ya Qajar hadi utawala wa kifalme wa Pahlavi, ilitekeleza kazi yake kwa kufanya mabadiliko ya kimsingi katika Katiba ya Iran. Kwa msingi huo utawala wa miaka 153 wa wafalme wa Kiqajari nchini Iran ulifikia kikomo na badala yake ukaanza utawala wa miaka 53 wa Pahlavi hapa nchini.

Majlisi ya Waasisi nchini Iran

Na miaka 173 iliyopita katika siku kama ya leo mwafaka na tarahe 5 Rabiul Thani mwaka 1267 Hijiria, gazeti la kwanza la lugha ya Kifarsi lililoitwa 'Waqai'e Itifaqiyeh' lilianza kuchapishwa mjini Tehran. Gazeti hilo lilianza kuchapishwa wakati wa kutimia mwaka wa tatu wa ufalme wa Nasiruddin Shah Kajjar, kwa amri ya Kansela Mirza Taqi Khan Amir Kabiri. Gazeti hilo lilikuwa likiandika habari za utawala wa wakati huo wa Iran, dunia na makala za kisayansi zilizokuwa zikitafsiriwa kutoka kwenye magazeti ya Ulaya. Gazeti la 'Waqai'e Itifaqiyeh' lilichapishwa hadi toleo nambari 472 na baada ya hapo likaendelea kuchapishwa kwa majina tofauti.

Waqai'e Itifaqiyeh