Dec 14, 2018 23:08 UTC
  • Jumamosi, Disemba 15, 2018

Leo ni Jumamosi tarehe 7 Mfunguo Saba Rabiu Thani 1440 Hijria sawa na tarehe 15 Disemba 2018 Miladia.

Siku kama yya leo miaka 208 il iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, aliaga dunia Abul Fadhl Hamdun Ibn Abdul Rahman mashuhuri kwa jina la Ibn Haj, mfasiri, mwanafasihi na fakihi mkubwa wa Kiislamu.  Alizaliwa huko nchini Morocco. Ibn Haj alijifunza elimu za fasihi na masomo ya dini kwa maustadh mashuhuhuri wa zama hizo na katika safari yake ya hija alikutana na kufahamiana na wanazuoni wakubwa kama Sheikh Murtadha Ansari na kusoma kwao. Alimu huyo ameacha vitabu vingi alivyoalifu katika elimu za fikihi, itikadi, tafsiri, mantiki na elimu nyingine.   ***

Abul Fadhl Hamdun Ibn Abdul Rahman mashuhuri kwa jina la Ibn Haj,

Katika siku kama ya leo miaka 186 iliyopita alizaliwa Alexandre Gustave Eiffel mhandishi na msanifu wa mnara mashuhuri wa Eiffel. Umashuhuri wa Alexandre Gustave unatokana zaidi na usanifu na uhandisi wake kwa mnara wa Eiffel mjini Paris. Mnara wa Eiffel una urefu wa mita 324 ambapo katika zama zakke ulikuwa mnara mrefu zaidi duniani. Alexandre Gustave Eiffel aliaga dunia tarehe 27 Desemba 1923 akiwa na umri wa miaka 91. ***

Alexandre Gustave Eiffel

Miaka 63 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Hujjatul Islam Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani. Msomi na alimu huyo wa Kiirani aliyekuwa mmoja wa watoa waadhi na makhatibu mashuhuri katika zama zake alikuwa na azma na irada imara ya kueneza na kufikisha maarifa ya Uislamu na Ahlul-Beit (as). Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani alikuwa akitoa mihadhara mjini Mash'had Iran na katika miji mingine na kadhalika katika Haram ya Imam Hussein (as) katika mji wa Karbala na Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) huko Najaf, Iraq. Hatimaye akiwa na umri wa takribani miaka 82 aliaga dunia katika siku kama ya leo na kuzikwa katika Haram ya Imam Ali bin Mussa al-Ridha (as) mjini Mash'had. ***

Hujjatul Islam Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani.

Siku kama ya leo miaka 62 iliyopita,  alifariki dunia Walt Disney shakhsia mashuhuri wa sekta ya filamu za watoto. Disney alizaliwa mwaka 1901 huko Marekani. Walt Disney alihitimu masomo katika Chuo Kikuu cha Havard na kutunukiwa shahada ya udaktari katika sayansi ya uchoraji na uchongaji (Fine Art). Disney alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha sanaa ya filamu za katuni. Mara kadhaa alitunukiwa tuzo za Oscar katika uwanja huo wa kutengeneza filamu za katuni. ***

Walt Disney

Na miaka 43 iliyopita katika siku kama ya leo sawa na tarehe 15 Disemba 1975, zilimalizika zama za udhibiti na ushawishi wa Uhispania huko Sahara ya Magharibi baada ya nchi hiyo kulazimika kuondoka katika eneo hilo. Polisario ni moja ya harakati za ukombozi wa Sahara Magharibi iliyowalazimisha Wahispania kukimbia eneo hilo. Harakati hiyo iliundwa mwaka 1973 baada ya wanamapinduzi wa Sahara kuasisi makundi kadhaa ya kupigania ukombozi wa eneo hilo.

Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Sahara Magharibi