Jan 18, 2019 23:39 UTC
  • Jumamosi, 19 Januari, 2019

Leo ni Jumamosi tarehe 12 Mfunguo Nane Jamadil Awwal 1440 Hijria mwafaka na tarehe 19 Januari 2019.

Siku kama ya leo miaka 487 iliyopita, alifariki dunia Ibn Tulun Dimashqi msomi mkubwa wa Kiislamu, aliyekuwa faqihi, mwanafasihi na mwanahistoria huko mjini Damascus, Syria. Ibn Tulun alizaliwa mwaka 880 Hijiria mjini Damascus na katika umri wake wote alifanya jitihada kubwa za utafiti, kufundisha na kuandika vitabu vya taaluma mbalimbali. Ibn Tulun Dimashqi ameandika vitabu vingi vya thamani kuhusiana na historia ya Kiislamu na pia katika uwanja wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu, hadithi, lugha, tiba na irfani. Aidha kitabu cha 'as-Safiinatu al-Tuluuniyyah' ni miongoni mwa athari za mwanazuoni huyo. ***

Ibn Tulun Dimashqi

Miaka 283 iliyopita katika siku kama ya leo, alizaliwa James Watt. mvumbuzi na mhandisi wa Kiingereza Msomi huyo alipendelea na kuvutiwa mno na utafiti kuhusu masuala ya kisayansi. Katika utafiti wake Watt alifanikiwa kuvumbua nishati ya mvuke na kuzusha mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda hususan usafirishaji wa nchi kavu na baharini. ***

James Watt

Katika siku kama ya leo miaka 221 iliyopita, alizaliwa Auguste Comte mwanafalsafa, mwanahisabati wa Kifaransa na mtaalamu wa falsafa umbile au positivism kwa kimombo. Comte alifikia daraja ya uhadhiri katika hisabati akiwa na umri wa miaka 18 tu. Vitabu mashuhuri vya mwanafalsafa huyo wa Kifaransa ni Auguste Comte and positivism na Early Political Writings. Comte aliaga dunia mwaka 1517. ***

Auguste Comte

Siku kama ya leo miaka 40 iliyopita, wananchi Waislamu wa Iran wenye imani na umoja walifanya maandamano makubwa kupinga mabaki yaliyosalia ya utawala wa kifalme Shah, yaani serikali ya Shapour Bakhtiar. Wafanya maandamano hao walitaka serikali hiyo ya kifalme itangazwe kuwa si halali, na pia kung'olewa utawala wa Shah na badala yale kuundwa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran. Siku hiyo Imam Khomeini MA akiwa mjini Paris alitoa ujumbe wa maandishi kwa wananchi wa Iran akisema kama: "Kwa uwezo wake Mola hivi karibuni nitaungana nanyi ili niweze kuwatumikia na kushirikiana bega kwa bega na matabaka yote ya wananchi kuelekea katika njia ya kujitawala na kuwa huru Iran."***

 Maandamano ya tarehe 29 Dei 1357

Miaka 9 iliyopita katika siku kama ya leo, Abdul Rauf Mahmoud al-Mabhuh, mmoja wa makamanda waandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS aliuawa shahidi huko Dubai, katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Mabhouh aliuawa na makachero wa Shirika la Ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel walioingia nchini Imarati wakitumia pasipoti bandia. Mabhuh alizaliwa katika familia iliyoshikamana na dini katika kambi ya Jabalia katika Ukanda wa Gaza, Palestina. Shahidi Mahmoud al-Mabhuh ni miongoni mwa waasisi wa Brigedi ya Izzudeen al-Qassam tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Baada ya kupita miezi kadhaa, Israel ilitangaza wazi kwamba, ilihusika na jinai ya kumuua Mabhuh. ***

 Mahmoud al-Mabhuh

Na siku ya leo tarehe 29 Dei inajulikana nchini Iran kwa anuani ya "Siku ya Gaza". Siku hii ni kumbukumbu ya kumalizika vita vya siku 22 vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza ambapo vita hivyo vilifikia tamati kwa ushindi wa muqawama na mapambano ya Kiislamu huko Gaza. Kutokana na vyombo vya Magharibi kuficha jinai za utawala haramu wa Israel na kwa upande mwingine kutokana na hamasa kubwa iliyooonyeshwa na wananchi madhulumu wa Gaza katika kutetea ardhi zao, siku hii imepewa jina la "Siku ya Kitaifa ya Gaza. ***

Siku ya Gaza