Mar 04, 2019 23:50 UTC
  • Jumanne tarehe 5 Machi 2019

Leo ni tarehe 27 Jumadithani 1440 Hijria sawa na tarehe 5 Machi mwaka 2019.

Siku kama ya leo miaka 192 iliyopita, sawa na tarehe 5 Machi 1827 alifariki dunia Alessandro Volta, mtaalamu wa fizikia wa Italia akiwa na umri wa miaka 83. Sambamba na kufundisha katika chuo kikuu, Volta alikuwa akifanya uhakiki na alifanikiwa kutengeneza chombo cha kupimia kiwango cha umeme Electrometre.

Alessandro Volta

Miaka192 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Pierre Laplace mwanahisabati mashuhuri wa kifaransa. Alizaliwa mwaka 1749 na baada ya kuhitimu masomo yake alijishughulisha na kufundisha  hisabati. Laplace alitumia sehemu kubwa ya umri wake kutwalii na kufanya uhakiki kuhusiana na elimu za nujumu na hisabati.

Pierre Laplace

Tarehe 5 Machi miaka 66 iliyopita alifariki dunia Joseph Stalin, kiongozi na dikteta wa Urusi ya zamani. Stalin alizaliwa mwaka 1879 nchini Georgia na alijiunga na mrengo wa kikomunisti baada ya kusoma fikra za mrengo huo. Joseph Stalin alipelekwa uhamishoni huko Siberia mwaka 1913 kutokana na harakati zake za kisiasa dhidi ya serikali ya wakati huo ya Urusi. Stalin alibakia huko hadi baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Urusi mwaka 1917. Alipata vyeo vya ngazi za juu wakati wa uongozi wa Lenin na alishika uongozi wa nchi hiyo akiwa pamoja na wanasiasa wengine mashuhuri baada ya kufariki dunia Lenin. Mwaka 1927 Stalin aliwafutilia mbali wapinzani wake ndani ya chama na kuwa kiongozi asiye na mpinzani katika Chama cha Kikomunisti. Joseph Stalin aliendelea kuwafuta na kuwaangamiza bila ya huruma wapinzani wake ndani na nje ya chama hicho.

Joseph Stalin,

Siku kama ya leo miaka 52 iliyopita sawa na tarehe 14 Esfand mwaka 1346 kwa mujibu wa Kalenda ya Kiirani, alifariki dunia Dakta Muhammad Musaddiq, Waziri Mkuu na mmoja wa wanasiasa mashuhuri wa Iran. Alizaliwa mjini Tehran mwaka 1261 Hijria Shamsia. Mwaka 1299 Hijria Shamsia ikiwa ni baada ya kuhudumu kama Waziri wa Fedha na Waziri wa Mambo ya Nje, Musaddiq alichaguliwa kuwa mwakilishi wa watu wa Tehran bungeni. Hata hivyo baada ya muda mfupi alijiondoa kwenye uwanja wa siasa na kurejea baadaye mwaka 1322.

Dakta Muhammad Musaddiq

Na siku kama ya leo miaka 3 iliyopita alifariki dunia mbunifu wa E-mail yaani baruapepe, Ray Tomlinson. Tomlinson ambaye mwaka 1971 alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja ya uhakiki kama mhandisi huko Boston nchini Marekani alianzisha mfumo wa awali wa E-mail katika mtandao wa Arpanet yaani nakala ya kwanza na intaneti. Mtaalamu huyo kwa hakika alituma baruapepe ya kwanza kabisa kwa mtindo wa kisasa. Ray Tomlinson alifariki dunia katika tarehe aliyozaliwa akiwa na umri wa miaka 75 kutokana na ugonjwa wa kiharusi. 

Ray Tomlinson