Mar 02, 2020 00:23 UTC
  • Jumatatu tarehe 2 Machi 2020

Leo ni Jumatatu tarehe 7 Rajab 1441 Hijria sawa na tarehe 2 Machi 2020.

Siku kama ya leo miaka 15 iliyopita, mwafaka na tarehe Pili Machi mwaka 2004, mamia ya watu wasio na hatia waliuawa shahidi na wengine kujeruhiwa katika miripuko kadhaa mikubwa iliyotokea katika maadhimisho ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) huko katika miji mitukufu ya Karbala na Kadhimein nchini Iraq. Katika mwaka huo wananchi Waislamu wa Iraq walifanya maadhimisho hayo kwa hamasa kubwa baada ya utawala wa dikteta Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa nchi hiyo aliyeng'olewa madarakani, kupiga marufuku kwa miaka kadhaa shughuli zote za aina hiyo. Miripuko hiyo ya kigaidi ya Karbala na Khadhimain ilitokea ikiwa ni muendelezo wa machafuko yaliyoikumba Iraq tangu nchi hiyo ivamiwe kijeshi na kukaliwa kwa mabavu na Marekani na Uingereza mwaka 2003.

Siku kama ya leo miaka 28 iliyopita alifariki dunia Bi. Kaukab Pur Ranjbar, mwalimu mkubwa wa Qur'an Tukufu. Kaukab Pur Ranjbar alizaliwa mwaka 1282 Hijiria Shamsia mjini Shiraz ambapo akiwa na umri wa miaka 16 alianza kukusanya nyaraka za namna ya kufundisha elimu za Kiislamu. Baada ya kuhitimu elimu ya msingi na kujifunza masomo ya Uislamu, alijishughulisha na kazi ya ualimu wa masomo ya dini huku akianza kuhakiki na kusahihisha chapa za Qur'ani za nchini Pakistan, India na nchi nyingine. Kadhalika Bi. Kaukab Pur Ranjbar mbali na kupitia maandishi ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na kuwa na uwezo mkubwa wa ufahamu wa lugha ya Kiarabu, pia alifanya juhudi kubwa za kufundisha Qur'ani kwa hatua nyepesi na ngumu. Alipofikisha umri wa miaka 27 alipatwa na maradhi ya upofu lakini akapona maradhi hayo baada ya kumuona Bibi Fatimatu Zahra (as) ndotoni na hivyo akayatolea wakfu maisha yake yote kwa ajili ya Qur'ani. Kwa miaka 46 alijipinda sana katika kazi hiyo sambamba na kuasisi vituo tofauti vya kidini ambavyo baadhi vilinasibishwa kwake. Aidha kuanzia mwaka 1338 hadi 1363 aliandika  kitabu cha juzuu sita kinachotoa mwongozo wa ufundishaji wa Qur'ani Tukufu kwa njia nyepesi. Aidha kitabu cha 'Mazungumzo ya Hassan na Hussein', ni kati ya athari za msomi huyo wa kike wa Iran. 'Bi. Kaukab Pur Ranjbar alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Siku kama ya leo miaka 63 iliyopita, nchi ya Morocco ilipata uhuru. Morocco iko kaskazini mwa Afrika katika ukingo wa Bahari ya Mediterranean na Bahari ya Atlantic na inapakana na Algeria na Sahara Magharibi. Ukoloni wa madola ya Ulaya dhidi ya nchi hiyo, ulianza tangu karne ya 15 Miladia. Mapambano ya wananchi Waislamu wa Morocco dhidi ya wakoloni wa Uhispania na Ufaransa yalipelekea nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1956.

Bendera ya Morocco

Siku kama ya leo miaka 123 iliyopita, mwanafizikia wa Kifaransa Henri Becquerel alivumbua mionzi ya nunurishi yaani radioactive. Henri alifikia mafanikio hayo baada ya kufanya tafiti katika mada za urani na vitu vinginevyo. Becquerel alikuwa akichunguza urani ndipo alipogundua mionzi hiyo. Utafiti wa mwanafizikia huyo wa Kifaransa ulimfanya atunukiwe tunzo ya amani ya Nobel mwaka 1903 na miaka mitano baadae aliaga dunia.

Henri Becquerel

Na katika siku kama hii ya leo miaka 1136 iliyopita alizaliwa mtaalamu wa hadithi na mwanafasihi wa Kiislamu Ibn Tataz, Abul Fat'h Mu'afi bin Zakaria bin Yahya. Ibn Taraz alikuwa miongoni mwa magwiji na maulamaa wakubwa wa madhehebu ya Shafi' na alitabahari sana katika elimu za fiqhi, fasihi, Hadithi na lugha ya Kiarabu. Msomi huyo wa Kiislamu ameandika vitabu vingi katika taaluma ya fiqhi. Miongoni mwa vitabu vya Ibn Taraz ni kile cha al Jaliis Wal Aniis. Bin Taraz alifariki dunia mwaka 390 Hijria akiwa na umri wa miaka 85 akiwa Baghdad nchini Iraq.