Jun 28, 2020 23:27 UTC
  • Jumatatu tarehe 29 Juni 2020

Lwo ni Jumatatu tarehe 7 Dhulqaada mwaka 1441 Hijria sawa na Juni 29 mwaka 2020.

Miaka 725 iliyopita katika siku kama ya leo alifariki dunia Ibn Baswis mtaalamu wa hati aliyejulikana kama Dimishki. Alizaliwa mwaka 651 Hijiria katika mji wa Damascus na kwa muda wa miaka 50 alijishughulisha kufundisha hati, na wakaazi wa mji huo walistafidi kwa elimu na sanaa kutoka kwake. Ibn Baswis aliandika hati kwa mitindo tofauti ya kupendeza na katika umri wake wa uzeeni aliandika nakala moja ya Qur'ani Tukufu kwa maji ya dhahaba kwa hati maridadi na za kupendeza. Qur'ani hiyo pamoja na athari nyingine za Ibn Basis bado ziko hadi leo. 

Miaka 107 iliyopita vilianza vita vya pili vya Balkan kati ya Bulgaria na muungano wa nchi za Serbia, Ugiriki, Montenegro, Romania na utawala wa Kiothmania. Bulgaria, Serbia, Ugiriki na Montenegro ambazo zilikuwa chini ya mamlaka ya Othmania karibu mwaka mmoja kabla ya hapo zilifanya uasi dhidi ya utawala huo na kufanikiwa kujikomboa kutokana na udhaifu wa watawala wa Kiothmania.

Vita vya Pili vyya Balkan

Miaka 44 iliyopita katika siku inayosadifiana na tarehe 29 Juni mwaka 1976, muungano wa visiwa vya Ushelisheli ulipata uhuru na kila inapowadia siku kama hii husherekewa visiwani humo kama siku ya taifa. Hadi kufikia katikati ya karne 18, wakati ambapo Wareno walikuwa wakiikalia kwa mabavu ardhi hiyo, visiwa vya Sychelles vilikuwa havijagunduliwa na havikuwa na watu wakazi. Kuanzia wakati huo Ufaransa nayo ikaanza kupenyeza nchini humo. Mwishoni mwa karne ya 18 wakati kulipopamba moto mapinduzi ya Ufaransa, wanajeshi wa Uingereza waliokuwa katika eneo la Afrika walivamia Ushelisheli. Mapambano ya kuikomboa nchi hiyo yalipamba moto tangu mwaka 1960 na kuendelea, na miaka 16 iliyofuata visiwa vya Ushelisheli au Sychelles vikapata uhuru na kuasisi mfumo wa Jamhuri. Ushelisheli inaundwa na visiwa kadhaa vilivyoko katika bahari ya Hindi huku ikipakana kwa karibu na jirani yake Madagascar.

Siku kama ya leo miaka 34 iliyopita ilianza operesheni ya kijeshi ya Karbala -1 kwa ajili ya kukomboa mji wa Mehran huko magharibi mwa Iran uliokuwa umetwaliwa na jeshi vamizi la Saddam Hussein wa Iraq. Mji huo ulikaliwa kwa mabavu muda mfupi baada ya jeshi la Baath na Iraq kuvamia ardhi ya Iran Septemba 1981 na ulikombolewa na wapiganaji shupavu wa Iran katika operesheni makini ya Karbala-1.

Operesheni ya Karbala -1