Jan 21, 2021 23:00 UTC
  • Ijumaa, 22 Januari, 2021

Leo ni Ijumaa tarehe 8 Jamadithani 1442 Hijria inayosadifiana na tarehe 22 Januari 2021.

Siku kama ya leo miaka 460 iliyopita inayosadifiana na tarehe 22 Januari 1561 alizaliwa mwanafalsafa na mtaalamu wa hesabati wa Uingereza Francis Bacon. Awali, Bacon alijishughulisha na masuala ya kisiasa na baadaye alikamatwa na kufungwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kula rushwa. Kipindi cha kufungwa jela kilikuwa fursa mwafaka kwa Francis Bacon kudhihirisha kipawa chake. Mwanafalsafa huyo alitoa mchango mkubwa katika kueneza sayansi asili nchini Uingereza na kuhuisha sayansi na falsafa barani Ulaya. Bacon ameandika vitabu kadhaa kikiwemo kile cha New Atlantis. Msomi huyo wa Uingereza alifariki dunia mwaka 1626.

Ayatullah Abu Abdullah Zanjani

Siku kama ya leo miaka 246 iliyopita, alizaliwa Andre Marie Ampere, mtaalamu wa hisabati na fizikia wa Ufaransa. Akiwa kijana mdogo alipendelea sana fani ya hesabati. Akiwa Chuo Kikuu cha Polytechnique cha mjini Paris, aligundua mambo kadhaa katika uga wa fizikia. Moja ya mambo aliyoyagundua Andre Marie Ampere ni pamoja na simu ya upepo "Telegrafu." Mtaalamu huyo alifariki dunia mwaka 1836.

Andre Marie Ampere

Siku kama ya leo miaka 120 iliyopita, alifariki dunia Alexandrina Victoria, malikia maarufu wa Uingereza akiwa na umri wa miaka 82. Victoria alizaliwa mjini London mwaka 1819 Miladia, huku akichukua nafasi ya William IV kiutawala ambapo alisalia katika madaraka kwa kipindi cha miaka 64. Katika utawala wa Alexandrina Victoria, kulishtadi ukandamizaji dhidi ya raia wa nchi hiyo. Kufariki dunia malikia huyo ilikuwa mwanzo wa kudhoofika utawala wa kifalme ambapo baada yake aliingia madarakani Edward VII.

Alexandrina Victoria

Katika siku kama ya leo miaka 65 iliyopita, alifariki dunia Ayatullah Sayyid Abdul Hussein Sharafuddin Aamili, alimu na msomi mkubwa wa Kiislamu. Ayatullah Sharafuddin alizaliwa mwaka 1290 Hijria huko Kadhimain moja kati ya miji ya Iraq. Alielekea Jabal Amil nchini Lebanon baada ya kuhitimu masomo yake na kuanza kujishughulisha na harakati za Kiislamu. Msomi huyo mkubwa ametoa huduma za thamani kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu na daima alikuwa akisisitiza suala la umoja baina ya Waislamu. Ayatullah Sayyid Abdul Hussein Sharafuddin ameandika vitabu na risala nyingi ili kufikiwa lengo hilo.

Ayatullah Sayyid Abdul Hussein Sharafuddin Aamili

Na siku kama ya leo miaka 42 iliyopita, inayosadifiana na 3 Bahman 1357 Hijria Shamsia, wakati ukikaribia ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu, iliundwa kamati kuu ya uratibu wa mapinduzi yenye lengo la kuzuia ghasia, machafuko na kujitokeza mpasuko kati ya safu ya wanamapinduzi. Kamati hiyo iliwataka wafanyakazi, wakulima , vibarua na wananchi kwa ujumla kuendeleza migomo na maandamano hadi pale utakapopatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Mapokezi ya Imam Ruhullah Khomeini