-
Hamas: Siku ya Quds inaukumbusha Umma majukumu yake ya kukomboa Msikiti wa al Aqsa
Apr 14, 2023 11:44Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa taarifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kutaka kuweko harakati ya kimataifa ili kuunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina na kuhitimisha uvamizi na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Qatar: Kuwaunga mkono Wapalestina ni kipaumbele katika sera zetu za nje
Apr 14, 2023 06:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema, kuwaunga mkono wananchi wa Palestina ni kipaumbele cha kwanza cha sera za nje za nchi hiyo.
-
Damascus: Shambulio dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa linaonyesha sura ya apartheid ya utawala wa Israel
Apr 13, 2023 08:09Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetangaza kuwa mashambulizi ya mara kwa mara ya walowezi wa Kizayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa ni matokeo ya ubaguzi wa rangi na tabia ya kigaidi ya utawala huo.
-
Netanyahu aamuru Mayahudi wasiingie Msikiti wa Al-Aqsa mpaka mwisho wa Ramadhani
Apr 12, 2023 12:48Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ametangaza kuwa kwa ushauri wa maafisa usalama wa Israel, Mayahudi wasiende katika Msikiti wa Al-Aqsa hadi mwisho wa mwezi wa Ramadhani.
-
Spika wa Bunge la Iran: Uchokozi wa utawala wa Israel unathibitisha utambulisho wake wa kifashisti na kibaguzi
Apr 11, 2023 03:03Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu, Bunge la Iran, amesema vitendo vya kichokozi vilivyofanywa hivi karibuni na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu vinadhihirisha tabia ya utawala huo wa kifashisti na ubaguzi wa rangi.
-
Al-Azhar yawataka Waislamu kuulinda Msikiti wa Al-Aqsa
Apr 09, 2023 11:28Taasisi ya Al-Azhar ya Misri imetoa wito kwa Waislamu wote kuulinda na kuutetea Msikiti wa Al-Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Qatar: Israel inabeba dhima ya kuenea vitendo vya utumiaji mabavu katika msikiti wa al-Aqswa
Apr 08, 2023 07:58Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imetangaza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unabeba dhima ya kuenea vitendo vya utumiaji mabavu katika msikiti wa al-Aqswa kutokana na hatua za kichochezi za utawala huo vamizi
-
Mufti wa Oman asisitiza udharura wa kuungwa mkono Wapalestina ili kuzuia hujuma za Wazayuni
Apr 07, 2023 02:21Mufti wa Oman ametoa amepinga vikali hujuma zinazoendelea kufanywa na Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina katika Msikiti Mtukufu wa al Aqsa na ametaoa wito wa kuungwa mkono Palestina.
-
Palestina: Hatutakubali msikiti wa Al-Aqsa ugawanywe kimatumizi kwa wakati na eneo
Apr 06, 2023 07:25Mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema: Hatutakubali msikiti wa Al-Aqsa ugawanywe kimatumizi kwa sura ya muda maalumu wa utumiaji na sehemu maalumu ya kutumia jambo ambalo wavamizi na walowezi wa Kizayuni wanapigania kulilazimisha liwe.
-
HAMAS: Damu za mashahidi zitalinda utambulisho wa msikiti wa al-Aqswa
Apr 01, 2023 09:22Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, damu mashahidi wa Palestina italinda utambulisho wa Kipalestina, Kiarabu na Kiislamu wa msikiti mtakatifu wa al-Aqswa.