-
SAUTi, Raia wa Burundi waitaka serikali kudhamini mifuko ya makaratasi kabla ya kuzuia ile ya plastiki
Aug 30, 2018 12:29Baada ya Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kusaini sheria inayopiga marufuku matumizi na biashara ya mifuko ya plastik nchini humo, wananchi wamekuwa wakihimizwa kuachana na matumizi ya mifuko ya aina hiyo ambayo inaharibu mazingira kwa kiasi kikubwa.
-
Wahitimu vyuo vikuu Burundi wahimizwa kujiajiri + Sauti
Aug 23, 2018 12:24Serikali ya Burundi imekuwa ikiwahimiza vijana walioshindwa kuendelea na elimu ya chuo kikuu kujiunga na kazi mbali mbali za kiufundi nchini humo katika dhamira ya kukabiliana na ukosefu ajira. Kwa maelezo kamili tumtegee sikio ripota wetu wa mjini Bujumbura, Hamida Issa
-
Rwanda na Burundi zashirikiana katika kuzuia ugonjwa hatari wa Ebola
Aug 08, 2018 00:13Serikali za Rwanda na Burundi zimeweka mikakati kabambe ya pamoja kwa ajili ya kupambana na maradhi hatari ya Ebola ambayo yameripotiwa katika eneo la Maziwa Makuu.
-
SAUTI, Burundi yakosoa kitendo cha Rwanda cha kuwatimua wakimbizi wa Kirundi bila kuwapa mali zao
Jun 28, 2018 11:14Serikali ya Burundi imekosoa kitendo cha serikali ya nchi jirani ya Rwanda cha kuwafukuza zaidi ya wakimbizi 550 bila sababu.
-
Afisa wa serikali na Wafaransa 4 watiwa nguvuni kwa ufisadi Burundi
Jun 24, 2018 08:20Serikali ya Burundi imemtia nguvuni afisa mmoja wa ngazi ya juu wa nchi hiyo na raia wanne wa Ufaransa kwa tuhuma za kufanya utapeli.
-
Nkurunziza asema hatogombea urais nchini Burundi mwaka 2020+SAUTI
Jun 07, 2018 11:00Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametangaza kuwa hatagombea urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020, licha ya katiba mpya aliyoiidhinisha hii leo kumpa kibali cha kusalia madarakani hadi mwaka 2034.
-
Franc bilioni 17 zimeshakusanywa Burundi kwa ajili ya uchaguzi + Sauti
Jun 05, 2018 12:15Serikali ya Burundi imetangaza kiwango cha Franc bilioni 17 za nchi hiyo sawa na dola milioni 17 za Kimarekani kuwa ndizo tayari zimekusanywa katika michongo inayotolewa ndani ya nchi hiyo kugharamia uchaguzi mkuu wa 2020. Hamida Issa na maelezo zaidi...
-
AU yatakiwa kuongoza mazungumzo ya amani ya Burundi
Jun 02, 2018 03:37Mabalozi wa nchi za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika katika Umoja wa Ulaya wameutaka Umoja wa Afrika uingie usukani katika mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa unaozidi kutokota nchini Burundi.
-
Mahakama yatupilia mbali kesi ya upinzani kuhusu kura ya maoni Burundi
May 31, 2018 10:28Mahakama ya Katiba ya Burundi imetupilia mbali kesi iliyowasilisha na muungano wa upinzani nchini humo kupinga matokeo ya kura ya maoni ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi, yaliyoipa ushindi kambi ya serikali.
-
Upinzani Burundi waenda mahakamani kupinga matokeo ya kura ya maoni
May 25, 2018 03:04Muungano wa upinzani nchini Burundi unaoongozwa na Agathon Rwasa jana Alkhamisi ulienda mahakamani kupinga matokeo ya kura ya maoni ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi, yaliyoipa ushindi kambi ya serikali.