-
Jeshi la Misri laangamiza wanachama 24 wa Daesh eneo la Sinai
Oct 16, 2017 04:32Jeshi la Misri limetangaza habari ya kuwaua wanachama 24 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika Peninsula ya Sinai, kaskazini mwa nchi.
-
Maghala kadhaa makubwa ya silaha za Marekani na Israel yagunduliwa katika maficho ya Daesh Syria
Oct 15, 2017 10:48Maghala kadhaa makubwa ya silaha za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel yamegunduliwa katika maficho ya genge la kigaidi la Daesh (ISIS) katika mji uliokombolewa wa al Mayadin mkoani Dayr al-Zawr, mashariki mwa Syria.
-
Nasrullah: Marekani inazuia kuangamizwa kikamilifu kundi la kigaidi la Daesh
Oct 09, 2017 00:18Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inazuia kuangamizwa kikamilifu kundi la kigaidi la Daesh huko Syria na inalisaidia kundi hilo kwa silaha kupitia kituo chake cha jeshi huko Syria.
-
Iraq kuwahukumu wanachama wa ISIS, raia wa Ulaya
Oct 08, 2017 10:42Vyombo vya mahakama nchini Iraq vinatazamiwa kuwatolea hukumu ikiwemo hukumu ya kifo, makumi ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) raia wa nchi za Ulaya.
-
Jeshi la Iraq laukomboa mji wa Hawija kutoka makucha ya ISIS
Oct 05, 2017 04:34Jeshi la Iraq limetangaza kuukomboa mji wa kistratijia wa Hawija kutoka katika makucha ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
-
Makamanda 7 wa Daesh waangamizwa katika mashambulizi ya ndege za kivita za Russia huko Syria
Oct 03, 2017 10:59Wizara ya Ulinzi ya Russia leo imetangaza habari ya kuuawa makamanda saba wa kundi la kigaidi la Daesh katika mashambulizi ya anga ya ndege za kivita za nchi hiyo huko Syria.
-
Iran: Kujitenga Kurdistan na Iraq kutalipa nguvu Daesh na Israel
Oct 01, 2017 11:56Hussein Amir-Abdullahian, Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kimataifa ya Bunge la Iran amesema hatua ya Massoud Barzani, Rais wa Serikali ya Eneo la Kurdistan ya kushinikiza kujitenga eneo hilo na serikali kuu ya Iraq ni sawa na kulishajiisha kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh na kutumikia maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Russia yaua zaidi ya magaidi 2300 katika kipindi cha siku 10 nchini Syria
Oct 01, 2017 00:23Wizara ya Ulinzi ya Russia imeashiria kushindwa vibaya magaidi wa Daesh (ISIS) na Jabhatunnusra nchini Syria na kusema kuwa, ndege za kivita za Russia zimeua magaidi 2,359 na kujeruhi wengine 2,700 katika kipindi cha siku kumi zilizopita.
-
Makumi ya shule zafungwa na magaidi wa Daesh nchini Afghanistan
Sep 14, 2017 00:12Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) limefunga shule 73 katika mkoa wa Jozjan, kaskazini mwa Afghanistan sambamba na kupora vifaa vya masomo.
-
Aslimia 85 ya ardhi ya Syria imekombolewa toka mikononi mwa magaidi
Sep 12, 2017 22:02Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema jeshi la Syria limefanikiwa kukomboa asilimia 85 ya ardhi yake iliyokuwa ikidhibitiwa na magenge ya kigaidi.