-
Uganda yachukua tahadhari kuhusu Ebola kabla ya uchaguzi DRC
Dec 21, 2018 11:18Uganda imeongeza kiwango cha tahadhari kuhusu ugonjwa wa Ebola, ili kukabiliana na wimbi tarajiwa la wakimbizi iwapo vurugu zitaibuka katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
-
WHO: Kesi 36 mpya za Ebola ziripotiwa DRC
Nov 30, 2018 01:03Hatari wa kuenea ugonjwa habari wa Ebola imeongezeka huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na katika nchi zinazopakana nayo baada ya kesi nyingine 36 kugunduliwa karibu na mpaka wa nchi hiyo katika wiki iliyomalizikia kwenye Novemba 29.
-
Wizara ya Afya: Ugonjwa wa Ebola umeibuka tena katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Nov 11, 2018 01:06Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, watu wasiopungua 319 wamethibitishwa kuambukizwa maradhi ya Ebola ikiwa ni wimbi jipya la maradhi hayo katika nchi hiyo.
-
UN:Hatua mpya zinafanikisha vita dhidi ya Ebola DRC
Nov 09, 2018 04:28Hatua mpya za kukabiliana na changamoto za vita dhidi ya mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC zinazaa matunda ingawa mlipuko huo bado unasalia kuwa hatari.
-
Uganda kuanza kutoa chanjo ya Ebola kwa wafanyakazi wa sekta ya afya
Nov 02, 2018 23:26Uganda imetangaza kuwa Jumatatu ijayo itaanza kutoa chanjo kwa baadhi ya wafanyakazi wake wa huduma ya afya dhidi ya maradhi ya Ebola. Hatua hiyo inachukuliwa kutokana na kuongezeka wasiwasi juu ya uwezekano wa kuenea hadi Uganda homa hiyo ya kuvuja damu inayosababishwa na virusi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo inapambana na mlipuko wa Ebola.
-
Wasiwasi wa WHO kuhusu ongezeko la maambukizi mapya ya Ebola DRC
Nov 02, 2018 02:32Shirika la Afya Duniani WHO limeeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya Ebola yaliyothibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC katika wiki nne zilizopita.
-
Baraza la Usalama lapasisha azimio la kupambana na Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Oct 31, 2018 04:47Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha kwa kauli moja azimio la kupambana na ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Uchunguzi: Mlipuko wa Ebola magharibi mwa Afrika umesababisha hasara ya dola bilioni 53
Oct 24, 2018 23:04Virusi vya Ebola vilivyozikumba nchi za magharibi mwa Afrika hususan Sierra Leone, Guinea and Liberia mwaka 2014 vilisababisha hasara inayokadiriwa kufikia dola bilioni 53.
-
WHO kuunda kamati ya kujadili mlipuko wa Ebola Congo DR
Oct 16, 2018 04:39Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa litaitisha kikao cha kamati ya dharura ya kuamua iwapo mlipuko wa sasa wa maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni mgogoro wa umma unaoitia wasiwasi jamii ya kimataifa au la.
-
Visa vipya vya Ebola vyathibitishwa Kongo DR
Oct 07, 2018 04:15Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha habari ya kugunduliwa kwa kesi tano mpya za maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola katika mji wa Beni, mashariki mwa nchi.