-
Watu 200,000 wapata chanjo ya Ebola nchini DRC
Aug 25, 2019 21:48Watu zaidi ya 200,000 wamepata chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia (DRC) ya Kongo katika mwezi huu wa Agosti.
-
Burundi yaanza kutoa chanjo ya Ebola kwa wahudumu wa afya
Aug 15, 2019 07:32Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa serikali ya Burundi imeanza kutoa chanjo ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola kwa wahudumu wa afya hususan wale wanaofanyakazi karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
SADC kuisaidia DRC kukabiliana ugonjwa wa Ebola
Aug 13, 2019 02:39Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC zimeunganisha nguvu kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
-
UN: Watu 86 wanaambukizwa Ebola kila wiki DRC
Aug 10, 2019 03:05Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Dunaini (WHO) limetangaza kuwa kwa wastani watu 86 wanaambukizwa ugonjwa wa Ebola kila wiki nchini Jamhuri ya Kdemokrasia ya Congo, DRC katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.
-
Rwanda na DRC kushirikiana katika kukabiliana na Ebola
Aug 07, 2019 07:02Serikali za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeazimia kushirikiana katika kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola.
-
Kesi 12 mpya za maradhi ya Ebola zaripotiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Aug 03, 2019 22:38Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, kumegunduliwa kesi mpya 12 za maambukizi ya maradhi ya Ebola katika mji wa Goma.
-
Congo DR yazidisha jitihada za kudhibiti Ebola mashariki mwa nchi hiyo
Aug 03, 2019 07:14Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanzisha juhudi kubwa za kudhibiti ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola huko mashariki mwa nchi hiyo baada ya mchimba migodi mmoja aliyekuwa na familia kubwa kuaga dunia kutokana na homa ya ugonjwa huo katika mji wa Goma.
-
Wasiwasi wa kuenea tena maradhi ya Ebola watawala Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Aug 01, 2019 23:44Wasiwasi wa mlipuko mpya wa maradhi ya Ebola umetanda katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya kuripotiwa visa vitatu vipya vya maambukizi ya maradhi hayo.
-
Rwanda yafunga mpaka wake na Congo DR kwa kuhofia virusi vya Ebola
Aug 01, 2019 08:18Serikali ya Rwanda imefunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kugunduliwa kesi ya tatu ya muathirika wa virusi vya ugonjwa wa Ebola katika mji wa mpakani wa Goma.
-
WHO yatangaza Ebola kuwa 'dharura ya kiafya duniani'
Jul 18, 2019 22:04Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa ni ''dharura ya kiafya inayohitaji jumuia ya kimataifa kuitazama''.