Aug 26, 2019 02:18 UTC
  • Watu 200,000 wapata chanjo ya Ebola nchini DRC

Watu zaidi ya 200,000 wamepata chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia (DRC) ya Kongo katika mwezi huu wa Agosti.

Katika taarifa siku ya Jumapili, serikali ya DRC imesema inatumai kuwa chanjo hiyo utaweza kukabiliana na mlipuko wa sasa wa Ebola ambao ni wa pili kwa maangamizi katika historia ya ugonjwa huo.

Taarifa ya Kamati ya Ebola katika serikali ya DRC imeonyesha kuwa, watu 204,044 wamepata chanjo ya Ebola aina ya Merck tokea Agosti nane. Tokea mlipuko mpya wa Ebola uripotiwe nchini DRC Agosti mwaka jana, takribani watu 2000 wamepoteza maisha na wengine 2,950 hivi sasa wameabukizwa ugonjwa huo.

Idadi hiyo ya waliofariki ni ya pili katika historia ya ugonjwa huo baada ya mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi baina yam waka 2014-2016 wakati watu wapatao 11,300 walifariki.

Maafisa wa afya wanaokabiliana na Ebola

Hayo yanajiri wakati ambao Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, virusi vya maradhi hatari ya Ebola vimeripotiwa kuenea katika maeneo mpya huko mashariki mwa DRC.

Michael Ryan, Mkurugenzi Mtendaji wa masuala ya dharura katika Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa, maeneo mawili ya Mwenga huko Kivu Kusini na Pinga huko Kivu Kaskazini yameripotiwa kuenea virusi vya maradhi ya Ebola

 

Tags