-
Ethiopia yaendelea kuwaachia huru mamia ya wafungwa wa kisiasa
Feb 09, 2018 10:48Mwanasheria Mkuu wa Ethiopia ametoa agizo la kuachiwa huru mamia ya wafungwa wa kisiasa, akiwemo mmoja wa viongozi mashuhuri wa upinzani nchini humo.
-
Mapigano Ethiopia yapelekea milioni moja kuwa wakimbizi
Feb 06, 2018 11:36Mapigano baina ya makabila mawili makubwa Ethiopia yamepelekea watu zaidi ya milioni moja kukimbia makao yao.
-
Ethiopia yawaachia huru wafungwa wengine zaidi ya elfu 2 wa kisiasa
Jan 27, 2018 04:11Serikali ya Ethiopia imeendeleza wimbi la kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, mara hii ikiwaondoa gerezani maelfu ya wafungwa waliotuhumiwa kuhusika na machafuko yaliyolikumba eneo la Oromiya kati ya 2015 na 2016.
-
Upinzani Ethiopia wataka kufanyika mazungumzo ya kitaifa
Jan 24, 2018 23:30Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Ethiopia ametoa wito wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa kuhusu mgogoro wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini humo.
-
Ethiopia yakataa upatanishi wa Benki ya Dunia katika mgogoro wake na Misri
Jan 22, 2018 22:59Waziri Mkuu wa Ethiopia amekataa pendekezo la Misri la kuitaka Benki ya Dunia kuwa mpatanishi katika mgogoro wa ujenzi wa bwawa unaofanywa na serikali ya Addis Ababa juu ya Mto Nile.
-
Waasi 148 wajisalimisha kwa serikali nchini Ethiopia
Jan 22, 2018 01:08Serikali ya Ethiopia imetangaza habari ya kujisalimisha waasi 148 kwa vikosi vya usalama vya nchi hiyo.
-
Mabalozi wa Afrika UN wapendekeza Trump akutane na viongozi wa Afrika Ethiopia
Jan 19, 2018 03:54Mabalozi wanaowakilisha nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa wamependekeza Rais Donald Trump wa Marekani akutane na viongozi wa nchi za Afrika nchini Ethiopia mwezi huu kufuatia kauli chafu aliyotoa kwamba wahamiaji wanaoingia nchini Marekani kutoka Afrika na Haiti wanatoka kwenye nchi za "shimo la kinyesi".
-
Ethiopia yamuachia huru kinara wa upinzani, wafungwa 115
Jan 17, 2018 11:37Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Ethiopia ambaye alikuwa gerezani ameachiwa huru, ikiwa ni jitihada za serikali za kutekeleza ahadi yake ya kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa.
-
Ethiopia yafuta mashtaka dhidi yawafungwa wa kisiasa
Jan 16, 2018 03:56Mwanasheria Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa serikali ya nchi hiyo imefuta mashtaka dhidi ya mmoja wa viongozi wa kambi ya upinzani na wapinzani wengine 528 wanaoshikiliwa katika magereza ya nchi hiyo.
-
Libya yawatia mbaroni wahajiri 81 kutoka Somalia, Ethiopia na Eritrea
Jan 12, 2018 10:15Vyombo vya usalama mashariki mwa Libya vimewakamata makumi ya wahajiri raia wa Somalia, Eritrea na Ethiopia, ambao walikwepa mtego wa magendo ya binadamu.