-
Ellen Sirleaf: Yahya Jammeh hayuko tayari kuachia madaraka
Dec 14, 2016 07:37Wakuu wa nchi za magharibi mwa Afrika ambao wamefanya safari huko Gambia kwa lengo la kusuluhisha mgogoro wa ndani uliojitokeza, jana walitangaza kuwa jitihada zao za kumshawishi Yahya Jammeh akabidhi madaraka bado hazijazaa matunda.
-
Timu ya upatanishi yaelekea Gambia kusuluhisha mzozo wa urais
Dec 13, 2016 08:13Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf anaongoza timu ya upatanishi inayotazamiwa kuelekea nchini Gambia hii leo kujaribu kuupatia ufumbuzi mzozo wa uongozi ulioibuka nchini humo, baada ya Rais Yahya Jammeh kupinga matokoe ya uchaguzi wa rais.
-
Kuendelea kutokota mvukuto wa kisiasa nchini Gambia
Dec 13, 2016 02:46Askari wa vikosi vya usalama nchini Gambia wamesambazwa kwenye maeneo ya mji mkuu Banjul kufuatia hatua ya Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kukataa matokeo yanayoonesha kuwa alishindwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe mosi ya mwezi huu wa Desemba.
-
Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zamtaka Yahya Jammeh akubali matokeo ya uchaguzi
Dec 11, 2016 08:11Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zimemtaka Rais Yahya Jammeh wa Gambia kukubali matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika nchini humo mwanzoni mwa mwezi huu na hivyo kuandaa mazingira ya kukabidhi madaraka kwa njia ya Amani na ya kidemokrasia.
-
Ndege ya Rais wa Liberia yazuiwa kutua Gambia, Yahya Jammeh apinga matokeo
Dec 10, 2016 15:28Mamlaka za Gambia zimetangaza kuizuia kutua nchini humo ndege ya Rais Ellen Sirleaf Johnson ambaye pia ni Mwenyekiti wa hivi sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS.
-
Yahya Jammeh kukabidhi madaraka mwezi Januari
Dec 05, 2016 15:26Yahya Jammeh Rais wa Gambia aliyeangushwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni nchini humo angali yupo nchini humo na atakabidhi madaraka kwa rais mteule, Adama Barrow mwezi Januari mwakani. Hayo yameelezwa na Waziri wa Mawasiliano wa Gambia.
-
Rais mteule wa Gambia kuangalia upya suala la kujiondoa ICC
Dec 04, 2016 15:06Adama Barrow, Rais mteule wa Gambia amesema atatengue uamuzi wa mtangulizi wake aliyembwaga katika uchaguzi wa siku chache zilizopita Yahya Jammeh wa kuiondoa nchi hiyo katika Mkataba wa Roma uliobuni Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.
-
Mgombea wa upinzani ashinda kiti cha Urais Gambia
Dec 04, 2016 03:11Adama Barrow, mgombea wa muungano wa upinzani nchini Gambia amembwaga Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh katika uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo ambao matokeo yake hayakutarajiwa.
-
Yahyah Jammeh ashindwa vibaya katika uchaguzi wa rais Gambia
Dec 02, 2016 15:44Rais Yahyah Jammeh wa Gambia amekiri kushindwa katika uchaguzi wa rais nchini humo na kwa msingi huo kuhitimisha utawala wake wa miaka 22 katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Uchaguzi wa Gambia unafanyika leo, Rais Jammeh anawania kipindi cha tano cha uongozi
Dec 01, 2016 04:36Wananchi wa Gambia waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais wa nchi hiyo.