-
Mtoto wa Rais mteule wa Gambia afariki kwa kushambuliwa na mbwa
Jan 17, 2017 07:27Mtoto wa kiume wa Rais-mteule wa Gambia mwenye umri wa miaka minane amefariki dunia kwa kushambuliwa na mbwa katika mazingira ya kutatanisha, wakati huu ambapo baba yake yuko nchini Senegal.
-
Mali yamtaka Jammeh akabidhi madaraka kwa amani
Jan 15, 2017 07:17Rais Ibrahim Boubacar Keïta wa Mali amemtaka Rais Yahya Jammeh wa Gambia akabidhi madaraka kwa amani na azuie nchi yake kutumbukia kwenye machafuko.
-
Umoja wa Afrika waitishia Gambia
Jan 14, 2017 13:21Mgogoro wa kisiasa nchini Gambia umekuwa tata zaidi katika kukaribia tarehe ya kuapichwa rais mpya wa nchi hiyo. Kuhusiana na suala hilo Umoja wa Afrika (AU) umemtishia Rais wa Gambia kuwa hautamtambua rasmi kuwa rais halali tangu tarehe iliyoanishwa kwa ajili ya kufanyika sherehe za kumuapisha rais mteule wa nchi hiyo.
-
UNOWAS kuhakikisha Jammeh anaondoka madarakani nchini Gambia
Jan 14, 2017 07:29Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Afrika Magharibi amesema kunafanyika jitihada za kumshawishi Yahya Jammeh aliyeshindwa katika uchaguzi wa rais Gambia kuondoka madarakani na kumuachia mshindi, Adama Barrow, achukue hatamu za uongozi nchini humo.
-
Adama Barrow asema yuko tayari kufanya mazungumzo na Jammeh
Jan 13, 2017 08:07Mshindi wa uchaguzi wa Rais nchini Gambia, Adama Barrow amesema yuko tayari kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Yahya Jammeh, ambaye alipinga matokeo hayo.
-
Bunge la Wawakilishi Nigeria lafungua njia ya kumpa hifadhi ya kisiasa Rais wa Gambia
Jan 12, 2017 16:54Bunge la Wawakilishi la Nigeria leo limepiga kura kuidhinisha uamuzi wa kumpatia hifadhi ya kisiasa Rais Yahya Jammeh wa Gambia endapo atakubali kung'atuka madarakani.
-
Mahakama Kuu ya Gambia yakataa kusikiliza shauri la malalamiko ya uchaguzi
Jan 11, 2017 04:06Mahakama Kuu ya Gambia imetangaza kuwa katika hali ya sasa haiwezi kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusu malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
-
Waziri wa Gambia aihama serikali ya Rais Jammeh
Jan 10, 2017 16:26Waziri wa Mawasiliano wa Gambia Sheriff Bojang amesema ameamua kujiondoa kwenye serikali tangu rais Yahya Jammeh wa nchi hiyo alipokataa kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe mosi ya mwezi uliopita wa Desemba.
-
Mahakama kusikiliza ombi la Jammeh, Ecowas kurejea Gambia kesho
Jan 10, 2017 08:16Mahakama ya Kilele ya Gambia inatazamiwa hii leo kuanza kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais iliyowasilishwa na Rais Yahya Jammeh anayetaka matokeo ya uchaguzi yabatilishwe.
-
Nigeria: Viongozi wa ECOWAS kutoa 'uamuzi mkubwa' juu ya Gambia
Jan 07, 2017 08:06Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) wanatazamiwa hii leo kutoa kile kilichotajwa kuwa 'uamuzi mzito' kuhusiana na mgogoro wa kisiasa unaoikabili Gambia